ad

ad

BEN AFFLECK & JENNIFER GARNER WAJIANDAA KUACHANA BAADA YA MIAKA 10 YA NDOA YAO


Ben Affleck na Jennifer Garner.
BAADA ya kudumu katika ndoa kwa miaka 10 na kujaliwa kupata watoto watatu, wanandoa wa Hollywood, Ben Affleck na Jennifer Garner wametangaza kuwa wanajiandaa kuachana.

 Ben Affleck na Jennifer Garner wakiwa na watoto wao Violet, Seraphina na Samuel.
Katika taarifa waliyoitoa kwa vyombo vya habari, wanandoa hao waliomba usiri katika kipindi hiki wanapoelekea kufungua ukurasa mpya kwenye maisha yao.

“Baada ya kufikiria kwa muda mrefu na kujitafakari kwa umakini, tumeamua kuchukua maamuzi magumu ya kuachana.
Tutaendelea kupendana na kuwa marafiki pamoja na kushirikiana katika kuwalea watoto wetu watatu. Hayo ndiyo maoni yetu katika suala hili linalohusu familia yetu. Tunawashukuru kwa kutuelewa." - walieleza wanandoa hao katika taarifa yao.
Kwa miezi kadhaa, umekuwepo uvumi kwamba wanandoa hao wanataka kuachana ila hapakuwa na taarifa rasmi ya kuthibitisha uvumi huo.
Wanandoa hao wana watoto wawili wa kike ambao ni Violet, 9, Seraphina, 6, na wa kiume aitwaye Samuel, 3.

No comments

Powered by Blogger.