APOSTLE JOHN KOMANYA KUZIKWA JUMATANO MAKABURI YA SEGEREA, DAR
MAZISHI ya Askofu Mkuu na Mwanzilishi wa Kanisa la Cathedral of Joy
(CoJ), Apostle John Komanya, yanatarajia kufanyika Jumatano, Julai 8,
mwaka huu katika Makaburi ya Tabata-Segerea jijini Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa ma mchungaji msaidizi wa kanisa hilo, Abel John Kigeli, ilieleza kuwa Apostle Komanya alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kisukari pamoja na typhoid, na kwamba siku za nyuma alikuwa amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo alikuja kuruhusiwa baada ya kupata nafuu.

Kwa sasa msiba upo eneo la Tabata-Kisukulu, Dar.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN
Apostle John Komanya akiwa na mkewe.
Apostle Komanya alifariki dunia usiku wa kuamkia jana akiwa katika
Hospitali ya Hindu Mandal, jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa.Taarifa iliyotolewa ma mchungaji msaidizi wa kanisa hilo, Abel John Kigeli, ilieleza kuwa Apostle Komanya alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kisukari pamoja na typhoid, na kwamba siku za nyuma alikuwa amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo alikuja kuruhusiwa baada ya kupata nafuu.
Komanya akihubiri kanisani kwake.
Siku mbili nyuma ndipo alipozidiwa tena na hivyo kupelekwa Hospitali
ya Hindu Mandal, ambapo mauti yalimkuta. Marehemu ameacha mke na watoto
watatu ambao wako nchini Marekani, sehemu ambayo pia alikuwa akihudumu.Kwa sasa msiba upo eneo la Tabata-Kisukulu, Dar.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN

Post a Comment