UJAUZITO UMENIVURUGA SHEPU YANGU, TIWA SAVAGE
Mwanamuziki wa Nigeria, Tiwa Savage.
Lagos NigeriaMWANAMUZIKI Tiwa Savage wa Nigeria amelalamika kwamba ujauzito alio nao hivi sasa umevuruga shepu yake hasa kutokana tumbo kujitokeza.
Mrembo huyo ambaye anategemea kumzalia mtoto mumeweTunji ‘Teebillz’ Balogun, amesema kwenye akaunti yake ya Instagram kwamba pamoja na kufurahia hali hiyo, ujauzito una changamoto zake.
“Wakati wote unatamani uzae mtoto umwona na unakuwa unafurahi wakati anapojitingisha tumboni na unapofahamu kwamba sasa amelala.”Ni safari ya kufurahisha tangu ujauzito hadi mwisho wake,” aliandika.

Post a Comment