SHILOLE: SASA NAMZALIA NUH MZIWANDA
Kutoka kwenye mtima! Staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed
‘Shilole’ amefungukia ishu ya kumbebea mimba mpenzi wake, Naftal Mlawa
‘Nuh Mziwanda’ ili kuwafunga midomo wanawake wa mjini ambao wanamzengea
jamaa huyo.

“Kwa sasa nimepanga kumbebea mimba na kumzalia Nuh,” alisema Shilole au Shishi Baby.
Staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa katika pozi na mpenzi wake Nuhu Mziwanda.
Akizungumza, Shilole alitiriria kuwa, kwa
muda mrefu amekuwa akibanwa na kazi zake za muziki ambazo anafanya na
mpenzi wake huyo kiasi kwamba hawakufikiria kuhusu kupata mtoto mapema.“Kwa sasa nimepanga kumbebea mimba na kumzalia Nuh,” alisema Shilole au Shishi Baby.
Post a Comment