NAPE AZUA UTATA CCM...kwa namna yoyote ile, CCM itarudi Ikulu hata kama ni kwa bao la mkono
Katibu wa Itikati na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.
“...kwa
namna yoyote ile, CCM itarudi Ikulu hata kama ni kwa bao la mkono...”
kauli hiyo aliyoitoa Katibu wa Itikati na Uenezi, Nape Nnauye hivi
karibuni, imezua utata mkubwa kwa baadhi ya wanachama wa chama hicho
wakidai wameshindwa kung’amua kama alikuwa akikimaanisha Oktoba 25,
wataingia Ikulu kwa kuiba kura au la.
Nape
(pichani) alitoa kauli hiyo Juni 23, mwaka huu katika Viwanja vya
Nyehunge wilayani Sengerema, Mwanza alipokuwa akihutubia wananchi kwenye
mkutano wa hadhara.
Wakizungumza
na gazeti hili kwa sharti la kutotaja majinia yao, wakazi mbalimbali wa
Jiji la Dar ambao ni wafausi wa CCM, walitoa maoni yao kuhusu kauli
hiyo ambapo wengine walionesha kutokubaliana nayo huku wengine wakidai
wanaiunga mkono kwani kiongozi huyo hakumaanisha watashinda kwa kuiba
kura.
“Kwa
kweli amenistaajabisha sana aliposema tutashinda kwa bao la mkono. Hii
inaashiria kuna hujuma huwa inafanyika ili CCM ipate ushindi,” alisema
mpiga kura mmoja, mkazi wa Tandale jijini Dar.
“Tunashindwa
kumuelewa, kiongozi kama yeye inakuwaje anasema watashinda kwa bao la
mkono? Anamaanisha kwamba CCM itashinda kwa njia ambazo si halali?”
alihoji Ahmed Zuber mkazi wa Kimara-Baruti, Dar huku mkazi mwingine wa
Mwenge aliyejitambulisha kwa jina moja la Salehe akiteteta:
“Nape
hakuwa na maana mbaya, alimaanisha CCM ina mtaji mkubwa wa watu katika
maeneo ambayo vyama vingine havina na mbinu za ushindi zipo nyingi
lakini si wizi.”
Ili kuondoa utata huo, mwanahabari wetu alimpigia simu Nape alipopatikana, alifafanua:
“Mimi
nashangaa sijui huu utata unatoka wapi? Video ya mkutano ule imejieleza
wazi tena tumeisambaza mitandaoni ili wananchi wenyewe waone
nilichoongea na kilichoandikwa gazetini (siyo ya Global Publishers).
“Kamwe
CCM haiwezi kushinda kwa kuiba kura. Ingekuwa inaweza kufanya hivyo si
ingekuwa inakwenda kuiba Pemba? Mbona haifanyi hivyo?” alisema Nape.
CHANZO: GAZETI LA AMANI


Post a Comment