ad

ad

MBUNGE SUGU ASHINDA KESI, AKABIDHIWA MTOTO WAKE



Ni habari ambayo imeandikwa na gazeti ya Mwananchi June 23 2015 ikitokea Mahakamani Manzese Dar es salaam kuhusu kesi iliyokua imefunguliwa na Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi kuhusu mke wake wa zamani.

Taarifa inasema Mahakama ya Manzese imeamuru Mbunge Joseph Mbilinyi akabidhiwe mtoto wao kutokana na kesi aliyoifungua dhidi ya mke wake huyu akidai anamuharibu mtoto.
Hii habari imekuja siku kadhaa tu baada ya TUZO ZA KILI 2015 ambapo mke huyu wa zamani aliingia kwenye headlines kutokana na vazi alilokuwa amevaa.
Faiza & Mwanae Sasha.

SIELEWI JOSEPH AMESHINDAJE KESI- USHAHIDI WA PICHA PEKE YAKE SIONI KAMA UNATOSHA MIMI KUPOKONYWA MTOTO WANGU- MTOTO WANGU NI MDOGO SANA ANANIHITAJI SANA - NA SITA RUDI HATA IKIBIDI KUUZA KILA NILICHO NACHO KWA AJILI YA KUSIMAMIA HILI- SIJAPEWA NAFASI NIMEPELEKWA MAHAKAMANI IJUMAA NA LEO JUMANNE NIMEPEWA HUKUMU/ MWANANGU ACHUKULIWE..... HAPANA ! SITARUDI NYUMA NA HAITAKUA RAHISI NINAKATA RUFAA NA KUTAFUTA WAKILI WA KUNISIMAMIA HILI- MWANANGU ANASOMA VIZURI ANAISHI VIZURI NA NAAMINI KWENYE MIKONO YANGU YUKO SALAMA ZAIDI YA KOKOTE/ YAANI KUHUSU KUKOSA KUKAA NA MWANANGU NI BORA KUFA KULIKO KUISHI NIKIMUONA SASHA ANA LELEWA NA MAMA MWINGINE IKIWA MIMI MAMA YAKE NIKO HAI NA MAKINI KATIKA MALEZI YA MTOTO WANGU- NINA NDOTO NA MWANANGU NYINGI SANA - NAHITAJI KUISHI NAE YEYE NDIO KILA KITU KWENYE MAISHA YANGU/ NAMPENDA SANA MWANANGU NA SIJASHINDWA KUMLEA- NAONA UCHUNGU SANA KUPELEKWA MAHAKAMANI NA KUPOKONYWA MTOTO WANGU BILA SABABU ZA MSINGI . SITAOGOPA CHEO CHAKE CHA UBUNGE KAMWE- NITASIMAMA KAMA MAMA MWENYE HAKI KWA MTOTO WAKE ..MUNGU NAOMBA NIELEKEZE.NISIMAMIE NA UNIHUKUMIE HUU UKATILI NINAO FANYIWA NA BABA SASHA .....Alimaliza"Faiza Ally"..

No comments

Powered by Blogger.