ANETH AIPA PIGO SKYLIGHT BAND
ALIYEKUWA kiongozi wa bendi ya muziki wa Dansi, Skylight, Aneth Kushaba ameachana rasmi na bendi hiyo na kuacha pigo miongoni mwa mashabiki wake na wanamuziki wenzake.
Chanzo kinadai kuwa Aneth aliamua kuachana na bendi hiyo aliyodumu nayo kwa zaidi ya miaka mitatu kuwa maslahi yalikuwa madogo na pia kukosa maelewano kati yake na menejimenti ambayo ilikuwa haimtekelezei.
Alipotafutwa Aneth kueleza ukweli kama ameondoka, alisema;
“Ni kweli nimeachana na Skylight Band kwa kuwa nilikuwa nikivumilia sana kwa mambo mengi ambayo hayakuwa yakitekelezwa. Nimeona bora nikaanzishe bendi yangu kwahiyo itambulike kuwa sipo tena katika bendi hiyo,” alisema Aneth.
Alipotafutwa mmoja wa viongozi wa bendi hiyo, Justin Ndege alisema kuwa yupo kikaoni atafutwe baadaye lakini hata alivyotafutwa baadaye tena simu yake haikupatikana hewani.

Post a Comment