VAN GAAL ASEMA DE GEA ATABAKI MANCHESTER UNITED
Louis van Gaal amesema anaamini David de Gea ataipiga chini nafsi ya kujiunga na Real Madrid katika dirisha la usajili la kiangazi na kubakia Manchester United.

Kipa huyo amekuwa akihusishwa kwa kiasi kikubwa na safari ya kurejea Hispania licha ya ofa ya mkataba mpya Old Trafford itakayomwingizia pauni 200,000 kwa wiki. De Gea ana nafasi finyu ya kucheza mchezo wa mwisho dhidi ya Hull City Jumapili hii baada ya kuumia kwenye mechi dhidi ya Arsenal wikiendi iliyopita, lakini Van Gaal haamini kuwa mlinda mlango huyo amecheza mchezo wake wa mwisho Manchester United. "Naamini bado De Gea atabakia," alisema kocha huyo wa United.

"Kwanza tunapaswa kuangalia kama kweli De Gea anaondoka na baada ya hapo tunaweza tukaongea mambo mengine. "Nataka kumchezesha katika mchezo dhidi ya Hull kwasababu ya ukweli kuwa ningependa kuchezesha kikosi imara, na nadhani nina kikosi imara chini ya De Gea." Je ni kweli De Gea ataipiga chini ofa ya kujiunga na Real Madrid? ni jambo la kusubiri.

CREDIT: SALUTI 5.COM
Post a Comment