ad

ad

SINGANO ATEMBEA NA MKATABA WA SIMBA MFUKONI

UONGOZI wa Klabu ya Simba umemtega kiungo wake mshambuliaji, Ramadhan Singano ‘Messi’ kwa kumtaka atafakari kwa mara nyingine kuhusu dau la shilingi milioni 30 alilotajiwa badala ya shilingi milioni 50 anazotaka.



Singano ambaye alipandishwa kutoka kikosi cha Simba B, inaelezwa kuwa anatembea na mkataba aliopewa kwa kuwa anahitaji kutafakari kabla ya kusaini.Mtu wa ndani kutoka Simba, ameliambia gazeti hili kuwa uongozi umekataa dau analotaka na badala yake anatakiwa kukubali lile la shilingi milioni 30.
“Nia ya kumsajili ipo lakini anatakiwa achague moja, kama akikataa hiyo fedha wanayotaka kumpa basi wataachana naye, lakini mkataba anao na anatembea nao,” kilisema chanzo hicho.Wakati huohuo, habari za uhakika ni kuwa beki Hassan Isihaka amesaini mkataba wa miaka mitatu kuendelea kuichezea Simba.

No comments

Powered by Blogger.