ad

ad

SHILOLE: KINA MAMA WOTE NISAMEHENI

BAADA ya wiki kadhaa kupita tangu picha zake zisambae zikimuonesha gauni likiwa limevuka nakuachia ‘nido’ wazi, staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameibuka na kuwaomba radhi kinamama wote.  
Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Akipiga stori na Over The Weekend, Shilole alisema kuwa anajua kwamba kitendo hicho kimewakwaza wengi na hakukusudia kufanya jambo kama lile. “Nimejifunza mengi na naendelea tena kuomba msamaha kuwa tatizo hili halitajitokeza tena ,niwaombe radhi kina mama na mashabiki wangu,” alisema. Shilole alifanya tukio hilo alipokuwa jijini Antwepen, Ubelgiji kwenye shoo ambapo aliongozana na mpenzi wake,Nuh Mziwanda.

1 comment:

  1. "Allah anakupenda dada mrejee yeye Na uache maisha ya dunia kabla hujamaliza maisha yako yenye kuhesabika.fikiri maisha yenye mwanzo Na yasiyo Na mwisho yenye kutegemea matendo yako yakiwa mema yatakusaidia Na yakiwa maovu Ni mzigo kwako.Allah anakupenda ndio sababu akakuletea kipenzi chake mtume Muhammad S.A.W. Ili awe rehma kwako Na kwa viumbe wote,ametufunza mtume kuwa kila binaadam Ni mkosa Na mbora ktk hao Ni yule mwenye kutubu, Na akatufunza kuwa kila mmoja wetu aombe mwisho mwema, Naam dada Na wote wapendwa turudini kwa Allah kwa kubadili mfumo wa maisha yetu ,mfumo ambao hatuli ila kwa tendo la dhambi ,hatuvai ila kwa nguvu ya pesa ya dhambi Na mengi Sana ya dhambi tumefanya,kwakuwa tumepewa nafasi ya pumzi mpaka sasa basi tufanye maamuzi sahihi ya TOBA Na kutafuta njia mbadala ya maisha yetu kwa kuwa wabunifu.Kina mama Ni viumbe Tu walioumbwa Na Allah hivyo kabla ya kuwaomba Wao msamaha muombe kwanza Allah msamaha nae Ni mwingi wa msamaha .tunakupenda Na tushikane mkono kwa mkono hadi PEPONI"

    ReplyDelete

Powered by Blogger.