STEPHEN WASSIRA ATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS
Anawashukuru wageni waalikwa waliofika kwenye ukumbi kutoka sehemu mbalimbali kwa kuweza kufika na kumuunga mkono huku wakiwa na imani naye.
Anasema kumekuwepo minong'ono mingi kuhusu yeye kugombea urais,leo nimekuja mwanza kuvunja ukimwa na kuvunja ukimya na kutoa shauri la kutangaza nia ya kugombea urais kupitia CCM.
Kilichosababisha nigombee Urais
Haki kama raia ambayo ni ya kikatiba
- Aliingia bungeni akiwa na miaka 25 na katika umri wa miaka 27 aliteuliwa kuwa waziri mdogo wa Kilimo.
- Akiwa na miaka 30 Mwalimu Nyerere alimteua kuwa mkuu wa mkoa.
- Baadaye aliteuliwa kufanya kazi ubalozi wa Washington DC
- Mwaka 85 alirudi tena na kuchaguliwa kuwa mbunge wa Bunda na baadaye akateuliwa kuwa Mbunge kamili wa wizara ya Kilimo na chakula.
- Alichaguliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Pwani.
Nimeshindwa kuandika miaka aliyokuwa akiteuliwa na positions nyingine mbalimbali kutokana na spidi kuwa ndogo,nimeshindwa kwendana na kasi yake, HIVYO TUSAIDIANE KWA WALE WANAOMTIZAMA
- Anasema amepata kuteuliwa kuongoza sehemu mbalimbali maana marais wote wa awamu nne walikuwa na imani naye.
- Mtu anayetaka kugombea Urais lazima mtia nia ayajue mambo ambayo yanawakabiri watanzania.
** Naona kampa bango la Moja kwa moja Lowassa kuwa Ikulu hawezi kukabidhiwa Mla Rushwa, wanaukumbi wamelipuka na kuanza kuimba
..Sema baba,sema usiogope sema *10
Kasema Leo wakati akitangaza nia kwenye ukumbi wa BOT Mwanza, kaongeza kuwa mtu yeyote anayeitaka ikulu kwa pesa ni wa kuogopwa kama ukoma.
Wadau hili siyo dongo alilopigwa Lowassa?
- Wassira amemaliza kuhutubia mkutano
- Waandishi wa habari wamepata wasaa wa kuuliza maswali.
==
24: Mwandishi kamuuliza Wassira anawezaje kuwa Mwenyekiti wa CCM wakati yeye ni mpizania aliyeasi?
Jibu la Wassira: Kuniuliza kwenda upinzani ni sawa na kumuuliza dereva aliyepata ajali kuwa ataendelea na basi lile au jipya.
23: Maswali mbalimbali sasa kwa Mh. Stephen Wassira toka kwa Waandishi wa habari.
22: Mh Stephen Wassira amemaliza kuongea sasa baada ya kutangaza rasmi nia yake ya kugombea Urais wa Tanzania 2015.
21: Tutawekeza katika usalama na jeshi letu litakuwa dogo ila tutahakisha linakuwa bora na imara lenye nguvu.
20: Muajiriwa huwezi kuwa Tajiri maana mshahara wako ni Kula na uishe,ukiona muajiriwa Tajiri jiulize ameupata wapi?
19: Ikulu hamuwezi kuweka mla rushwa maana mkiweka mla rushwa pale siku nyingine atauza IKULU yenu .
18: Tangu mmenijua hamjawahi kusikia nina kashfa ya rushwa, ilipotajwa kashfa ya EPA na ESCROW zote sijahusishwa.
17: Hata serikali ya kijiji leo rushwa imetawala,unapoenda kuomba barua unaambiwa njoo kesho lengo lake umpe rushwa.
16: Nchi ina tatizo la rushwa, ninapozungumza rushwa lazima mnipime kama mimi ni mkweli, usizungumzie rushwa kama fasheni.
15: Nchi yetu ina tatizo kubwa la rushwa, ukikataa hili lazima kesho litakuumbua, unapozungumza hili itoke moyoni, usipinge Rushwa kwa fasheni tu ili watu wakuone.
14: Kuna watu wanalalamika tu kuhusu barabara, waswahili wanasema mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.Serikali ya Rais Kikwete imefanya mambo makubwa na mazuri.
13: Suala la afya ikiwezekana tutahakikisha kila Mtanzania anakuwa na bima ya afya kumuwezesha kupata matibabu.
12: Pia nitaboresha elimu yetu ili iwe ya kisasa zaidi na wasomi wetu waweze kupambana na soko la Afrika na Dunia.
11: Ninaamini sekta kubwa itakayowezesha ajira kwa vijana ni kilimo, muhimu ni kuwa na vifaa vya kisasa.
10: Ajira kubwa itakayoweza kuwakomboa vijana ni kuwezesha vijana kuwa wabunifu ili kuweza kujiajiri wenyewe.
9: Maendeleo ya mifugo yatazingatiwa ili kuhakikisha hii biashara inakua, pia kipaumbele katika kusimamia ardhi.
8: Serikali yangu itahakikisha uchumi wetu unaendelea kukua juu zaidi na Watanzania kuwezeshwa na kuendesha uchumi.
7: Nitasimamia utumishi wa umma uimarishwe zaidi na kuhakikisha unatoa shughuli zake kwa usahihi.
6: Nitahakikisha Mahakama, Serikali na Bunge zinaimarishwa.
5: Mambo ya msingi nitayozingatia kwenye uongozi wangu ni kuendeleza Tanzania imara, umoja, amani na mshikamano.
4: Baada ya kutafakari kwa muda nimeamua kugombea nafasi hii ya juu maana nimeona ni wakati sahihi kwangu.

Post a Comment