ad

ad

DAVINA AIPA LIKIZO NDOA YAKE

Mapumziko! Staa wa sinema za Kibongo, Halima Yahya ‘Davina’ amefunguka kuwa baadhi ya watu wanafikiria hatarudi kwenye ndoa yake lakini kwa upande wake anaamini kuwa anakula likizo fupi kisha atarejea kuendelea na maisha ya ndoa.
 
Halima Yahya ‘Davina’
Hivi karibuni, Davina aligombana na mumewe aliyehisi anaibiwa ‘mali’ zake na mwigizaji Mike Sangu.
Akizungumza  Davina alisema mfarakano katika ndoa ni jambo la kawaida hivyo watu wasikichukulie kama kitu kikubwa anaamini yatakwisha na watakaa sawa.
“Katika ndoa lazima mfarakano utokee, wanandoa wanaunamaliza na mimi naamini ninapozi kidogo nitarudi kwenye ndoa yangu, sijaachana na mume wangu ni matatizo tu yatapita na maisha yataendelea,” alisema Davina.

No comments

Powered by Blogger.