ad

ad

CHRIS BROWN ASHEREHEKEA MWANAYE KUTIMIZA MWAKA

 
Staa wa Pop, Christopher Maurice ‘Chris Brown’.
STAA wa Pop, Christopher Maurice ‘Chris Brown’ jana usiku alikuwa akisherehekea mwaka mmoja wa mtoto wake, Royalty.
 

Mtoto wake, Royalty.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Chris alimweka Royalty akiwa ametoka kuoga na ulimi akiutoa nje kisha akaambatanisha na maneno yaliyosomeka;
“Heri ya kuzaliwa mtoto wangu kipenzi Royalty!!!! Nakupenda.”
 

Mama wa mtoto Nia Guzman.
Chris amekuwa akimwanika mtoto wake katika mitandao ya kijamii mara kwa mara tangu mwezi Machi, mwaka huu baada ya kugundua kuwa ni mtoto wake aliyezaa na mwanamke aliyefahamika kama Nia Guzman.
Mapema wiki hii, mwanamke huyo alikuwa akigombana na Chris juu ya malezi ya mtoto wao huyo na kutaka apewe pesa nyingi ya kumlea kutoka dola 2,500 (sawa na shilingi milioni 4 na nusu za Kitanzania) hadi 15,000 (sawa na shilingi milioni 28 na nusu za Kitanzania) kwa mwezi.
Kwa upande wa Chris yupo katika harakati ya kuongezea jina la pili la mtoto huyo na kuliweka katika cheti chake cha kuzaliwa.

No comments

Powered by Blogger.