TIKO AMEKIMBIA NYUMBA YAKE KISA MAMBO YA KISHIRIKINA
MWANADADA kutoka tasnia ya filamu na muziki Bongo,
Tiko Hassan ameikimbia nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya Mwananyamala
jijini Dar kutokana na mambo ya kishirikina.Akizungumza hivi
karibuni Tiko alisema kuwa, ameamua kuihama nyumba hiyo licha ya kwamba
kodi yake haijaisha kufuatia maruweruwe yaliyokuwa yakimpata nyakati za
usiku.
“Yaani nimekuwa nikishindwa kulala kwa raha kwani usiku huwa nasikia sauti za ajabu, mara nahisi kuna watu wanatembea ndani, mara mapaka yanalia dirishani kwangu, kimsingi sikuwa nikiishi kwa amani, nimeona nihamie Kinondoni yasije yakanikuta makubwa,” alisema Tiko.

Post a Comment