MOURINHO AZIDI KUTIA UTAMBI LIVERPOOL KUHUSU RAHEEM STERLING
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amezidi kuchochoea moto mgogoro wa mkataba mpya wa mshambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling kwa kusema kama angekuwa yeye ‘angemruhusu’ mchezaji huyo aondoke.
Jose Mourinho ametoa kauli hiyo katika kipindi ambacho Raheem Sterling amesitisha mazungumzo ya mkataba mpya Liverpool akitaka jambo hilo lisubiri hadi mwisho wa msimu.
Raheem ameweka wazi kuwa shida yake sio pesa bali ni kusaka mataji.
Mourinho amesema kwake yeye sera ni moja tu – kuuza mchezaji yeyote ambaye hana utashi wa kuendelea kuitumikia klabu.
Kocha huyo amesema katika hilo huwa hajali jina wala thamani ya mchezaji. “Kama mchezaji hana nia ya kucheza chini yangu, huwa sisiti kumpiga bei.” Anaeleza Mourinho ambaye timu yake inatajwa kumwania Sterling.
Post a Comment