ad

ad

Kitanzi, Kisu au Bastola - 12



ILIPOISHIA…
“Ni mbinu za kikazi, siwezi nikakueleza. Cha msingi naomba unijibu maswali nitakayo kuuliza,” afande John aliyeyusha swali la Henry kwa kuhamisha mada.
ENDELEA…

“Haya uliza!” Henry alijibu kwa hasira baada ya kuona hakupata jibu zuri kutoka kwa afande John.
“Serenity inajihusisha na nini?”
“Come on! Afande John, nilidhani unajua kuhusu hilo, kwani hujui kama Serenity inawauza wasichana kwa wageni wa kizungu wanaokuja nchini?”
“What! Mimi nilitambua inahusika katika shughuli za urembo na kuwapromoti mamiss.”
“Wasichana wote wanaoonekana kama mamiss hutumikishwa kingono, Serenity ni danguro kubwa linalojiendesha kwa kivuli cha masuala ya urembo, hakuna lolote!”
“Mh! unauhakika na unachokiongea?”
“Yah, asilimia mia mbili,”
“Mmiliki wake ni nani?”
“afande mimi nawafahamu watu wawili tu; Mr. Chakos na Madam Flaviana lakini mmiliki wake nimewahi kusikia kuwa anajulikana kwa jina la Mr. George.
Hakuna mtu yeyote ambaye amewahi kuuona uso wake, hata Mr.Chakos mwenyewe hajawahi kuonana naye hata siku moja. Wanasema kuwa yeye ndiye hutafuta amtakaye na siyo wewe umtafute yeye. Mara zote Mr. George huongea kwa simu kwa sauti tofautitofauti au hutuma ujumbe kwa njia ya mtandao kwa watu maalumu tu. Kwa hiyo kumtafuta ni sawa na kuitafuta njia ya mauti,” alisema Henry ambaye maelezo yake yalizifanya nywele za afande John zisimame kwa hofu.
Mara nyingi nywele zake zinaposimama na kwa mtindo huo, afande John hukosa amani kwa kuwa hujua kuna hatari inamnyemelea, hatari yake kwa wakati huo ilikuwa ni hilo suala la Serenity.
***
NDANI YA UWANJA WA NDEGE, MAHALI FULANI
Waarabu wawili waliovalia suti na miwani myeusi walionekana kuteremka ngazi za ndege moja iliyoonekana kutua muda mchache uliopita. Mavazi na mienendo yao ilionekana wazi kuwa ni walinzi wa mtu au kitu fulani cha gharama. Kwa umakini mkubwa wakaangalia kila upande kisha mmoja wao akajongea mbele kidogo ambapo hapo walionekana Mr. Chakos na Madam Flaviana wakiwa na kundi la wasichana warembo waliokuwa wakitabasamu muda wote isipokuwa wasichana wawili pekee ambao ni Sonia na Carolina.
Baada ya Mwarabu yule aliyeonekana kama bodigadi kuwaona wenyeji wake, akatoa ishara kwa yule mwingine ambaye alichomoa simu yake na kupiga mara moja. Sekunde chache baadaye walionekana kuteremka Waarabu wengine ambao idadi yao ilifikia wanaume kumi na moja. Wengi walionekana kuvalia kanzu na vilemba vichwani isipokuwa mmoja tu kati yao ambaye alivalia kizibao cha rangi ya kahawia, miwani ya jua na kanzu nyeusi  kiasi cha kuonekana nadhifu kuliko wote waliokuwa hapo.
“Bila shaka yule ndiye mgeni wao,” alisema Henry aliyejificha ndani ya gari la vioo vya tintedi akimwambia afande John ambaye alikuwa bize akiliangalia tukio zima kwa darubini yake huku akivuta lenzi yake kuelekea upande waliosimama warembo wale. Kwa umakini mkubwa akapiga picha kadhaa za wasichana hao kwa kubonyeza kitufe fulani cha darubini hiyo ya kisasa na kusevu ndani yake kama picha za mnato.
“Unaweza kumtambua mmojammoja kama nikikuonesha picha zao?” aliuliza afande John baada ya kumaliza kuchukua picha ya kila mrembo aliyekuwa katika kundi lile.
“Yah,” alijibu Henry huku akiangalia kwa makini nje ya kioo chake.
 Yule Mwarabu nadhifu kuliko wote alionekana kujongea mbele na kuongea kwa muda na Mr.Chakos kisha wakapeana mikono na kukumbatiana kwa furaha kabla ya kila mmoja kumbusu mwenzake shavuni kama desturi ya Waarabu ilivyo.
Baada ya kitendo hicho Kwa unyenyekevu, Mr. Chakos na Madam Flaviana waliwaongoza wageni wao mpaka kwenye msururu wa magari ya kifahari yaliyoegeshwa nje ya uwanja huo na kuwabeba wageni hao wakielekea kuponda raha ndani ya jengo la Serenity.
Kila msichana aliyekuwa uwanjani hapo alipangiwa gari atakaloingia na kuketi akiwa na mgeni wake kabla ya baadaye kununuliwa na wageni hao ambao kwa huduma ya kila mrembo watapaswa kulipa fedha zisizopungua dola elfu mia tano kwa siku.
Wakati wakielekea Serenity, Sonia alikuwa ameketi siti ya nyuma kabisa na Mwarabu mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Awadh Sayeed. Muda wote Awadh alionekana kumsumbua Sonia kwa kumpapasapapasa kila mara.
Wakati mwingine alitumia nguvu kutaka kumvua blauzi yake kitendo ambacho Sonia alikichukia na kubaki akijisitiri mwili wake huku machozi yakimtoka.
Bila kujali, Awadh aliendelea kumnyanyasa mrembo huyo huku akionekana kuvutiwa na kitendo alichokuwa akikifanya.
Kuna wakati alimshika na kumpiga makofi huku akimtanua miguu yake kwa nguvu ili amalize haja zake humohumo kwenye gari, lakini Sonia alibana miguu yake kwa kadiri alivyoweza asiruhusu kudhalilishwa.
Walipofika Serenity, wengi kati ya waarabu hao waliondoka na warembo hao huku kila mmoja akielekea katika vyumba maalumu ambavyo vilikuwa tayari vimeandaliwa kwa ugeni huo.
Bila kupoteza muda Awadh aliyeonekana kuvutiwa na Sonia alikuwa wa kwanza kumbeba msichana huyo na kuingia naye ndani ya chumba chake tayari kwa kutekeleza azma yake mbaya.
Kwa mbali Carolina aliyekuwa akiingia chumbani kwake na Mwarabu mwingine aliyejitambulisha kama Omar Kareem, alimuona Sonia akihangaika kujinasua maungoni mwa Mwarabu huyo, moyo wake ulimuuma sana kwa kitendo kile lakini katika mazingira hayo hakuwa na cha kufanya zaidi ya kutafakari jinsi ya kuyaepuka matatizo yake kwanza kabla ya kumsaidia mwenzake.
***
Salima alionekana kuvinjari na Prince Khalfani kwa mtindo wa pekee. Mara alimkumbatia na kumbusu, mara alisimama na kuzungusha kiuno chake laini akicheza ala za kiarabu na mara nyingine aliongea kwa lugha laini na Prince Khalfani ambaye muda wote huo alikuwa mtulivu sana kama vile buibui atuliavyo akisubiri mdudu ajipeleke katika utando wake aanze kumshambulia.
***
Wakati mambo yote yakiendelea kama yalivyopangwa, Madam Flaviana na Mr. Chakos wote walikuwa makini kuhakikisha hakuna kitakachoharibu ugeni wao.
Wakakaa kwenye kompyuta zao wakiangalia kila kitu kinachofanyika katika vyumba hivyo. Katika kuonesha kwamba suala hilo lilikuwa na umuhimu, Mr. George mwenyewe alipiga simu kuulizia kila kitu kilichokuwa kikiendelea.
Wakati mwingine yeye mwenyewe ndiye alikuwa akitoa maelekezo ya nini kifanyike, wapi na wakati gani.
***
Carolina akiwa chumbani na Omar, alivua nguo zake taratibu na kuvaa mavazi mepesi ya usiku kama alivyotakiwa kufanya. Wakati huo Omar alikuwa kitandani ameegemea kitanda chake akivuta sigara yake kwa pupa huku akimtazama Carolina kwa jicho la husuda, Carolina alilishtukia na kuzidisha manjonjo.
Akili ya Carolina muda huo ilifanya kazi haraka sana kwani kadiri muda ulivyozidi kuyoyoma, ndivyo alivyozidi kupata wasiwasi juu ya rafiki yake Sonia ambaye kwa muda huo alikuwa katika wakati mgumu na Awadh.
Harakaharaka lakini kwa mpangilio, Carolina aliuchomoa udi wake ndani ya boksi maalumu, akauwasha kisha akaanza kuufukiza chumba kizima kama wafanyavyo watu wa Pwani.
Taratibu akajongea mahali alipolala huku akilipandisha gauni lake taratibu kana kwamba alijitoa kumpatia mwili wake.
Lakini kadiri alipokuwa akimsogelea ndivyo Omar alivyozidi kutetemeka kwa hofu, mara akadondoka kitandani kama gogo huku akitoa sauti ya kukoroma kana kwamba alipitiwa na usingizi mzito.
Baada ya zoezi hilo, Carolina alikimbilia bafuni ghafla na kunawa uso wake huku akijiziba pua kuuepuka moshi wa udi uliotanda ndani ya chumba hicho. Haraka  pasipo kupoteza muda aliuzima udi ule ambao vielelezo vyake vilionesha kuwa ulitengenezwa kwa sumu aina ya ‘Carbon Monoxide.’ Sumu ambayo huanza kwa kulegeza fahamu za mtu kisha kufuatiwa na usingizi mzito kabla ya kifo.
Kama mzimu, Carolina akazima taa na kurudi taratibu mpaka kwenye mabegi ya Omar. Akachambua nguo zake akitafuta simu au kifaa chochote cha mawasiliano ambapo kwa bahati aliipata simu ya kisasa ‘Smart Phone’ ambayo aliiwasha na kutuma ujumbe mfupi kwa mtu aliyemfahamu mwenyewe.
***
“Sikilizeni, nimetumiwa meseji ya hatari kutoka kwa afande Beatrice. Haya kaeni tayari kwa kuvamia!” alisema Afande John akiwaambia makachero wenzake ambao tayari walikuwa wameishaizingira ngome ya ‘Serenity.’
 “Samahani kidogo, Beatrice ndo nani?” Henry alishindwa kujizuia na kuamua kuuliza baada ya kusikia jina la afande Beatrice likitajwa kama mtu aliyetuma ujumbe wa hali ya hatari muda mfupi uliopita.
“Ni afisa upelelezi ambaye alijipenyeza ndani ya Serenity bila kujulikana,” alijibu afande John lakini jibu hilo lilizidi kumwacha Henry njia panda badala yake akauliza tena.
“Nini? Ina maana kumbe mlikuwa mnaifuatilia hii inshu kwa muda mrefu? Hivi huyo Beatrice ni nani humo ndani?”
“Ni siri za kikazi. Kukusaidia tu ni kwamba, ‘Beatrice’ siyo jina lake halisi kwa hiyo usijisumbue kufikiria kama unamfahamu au la. Hima tuoneshe njia,”
“Tuelekee huku,” aliongea Henry na kuingia kwenye mtaro wa majimachafu uliopita chini ya ukuta na kuibukia ndani ya uzio wa jengo hilo nyuma yake akifuatiwa na makachero ambao wote waliingia huku macho yao yakiwa makini kuangalia kila upande tayari kukabiliana na adui yeyote.
Kwa namna fulani waliweza kupenya hadi ndani kabisa ya jengo hilo bila kuonekana kwa kuwa kulikuwa na giza nene sana usiku huo. Mwanga pekee ulioonekana hapo ni ule uliotokana na taa zilizoonekana kutokea vyumba vya ghorofani na juu ya ukuta wa fensi ile ndefu.
***
Akiongozwa na hisia zake, Carolina alitoka chumbani kwake na kupita koridoni haraka kisha akaingia bila hodi ndani ya chumba alichokuwemo Sonia na yule Mwarabu Awadh.Wote walishtuka baada ya kumuona Carolina akiwa amesimama mbele yao. Aliyeshtuka zaidi alikuwa ni Awadh ambaye kwa wakati huo alikuwa kama alivyozaliwa.
“Maadha turidu (unataka nini)?” Awadh alifoka kwa kiarabu huku akimtazama Carolina kwa hasira.
“Laashakka (hakuna shaka),” alijibu Carolina kwa kiarabu pia huku akavifungua taratibu vifungo vya gauni lake jepesi akijaribu kumlaghai Awadh kwa mwili wake kana kwamba alikuwa na nia ya kufanya mapenzi ya watu watatu.
Wakati huo Sonia aliyekuwa amejikunja pembeni ya kitanda, akikikumbatia kipande cha nguo yake ambacho ndiyo pekee kilichokuwa kimebakia kumsitiri maungo yake, alibaki akimshangaa rafiki yake asijue kusudio lake.
ITAENDELEA KESHO

No comments

Powered by Blogger.