ad

ad

HATIMAYE ALLY CHOCKY ATAMBULISHWA RASMI TWANGA PEPETA


Kama Saluti5 ilivyokuwa imebashiri kuwa Ally Chocky atatambulishwa rasmi Twanga Pepeta muda mfupi ujao na ndivyo ilivyokuwa ambapo msanii huyo ametangaza kujiunga na bendi hiyo hivi punde kupitia mkutano wake na waandishi wa habari.

Katika mkutano huo uliofanyika Nemax Hotel, Kinondoni jijini Dar es Salaam, Chocky akasema ameamua kurejea Twanga Pepeta na kuahidi makubwa kwa mashabiki wa bendi hiyo.

Kama ilivyotarajiwa, Chocky ameambatana na dansa Super Nyamwela ambaye naye pia anarejea Twanga Pepeta.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na Asha Baraka, Luizer Mbutu na Omar Baraka,  Chocky akasema amerejea Twanga Pepeta bila shinikizo lolote na hana mpango wa kuhama tena bendi hiyo.

Onyesho la kwanza kwa Ally Chocky ndani ya Twanga Pepeta litafanyika tarehe 18 katika ukumbi utakaotajwa hapo baadae.

Chocky amesema ametua Twanga Pepeta na zawadi ya nyimbo tatu “Kichwa Chini”, “Usiyaogope Maisha” na “No Discussion”
  Luizer, Ally Chocky na Super Nyamwela
 Ally Chocky na Asha Baraka
 Ally Chocky Luizer na Super Nywamwela
CHANZO: SALUTI 5

No comments

Powered by Blogger.