BOZI: NAY WA MITEGO ANA LAANA YANGU NDO CHANZO CHA MIGOGORO YOTE!
MSANII wa filamu Bongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ amesema kuwa migogoro yote inayomtokea aliyewahi kuwa mwandani wake, Emmanuel Elibariki ‘Nay’ ni kutokana na laana ya kumsambazia picha zake za utupu.
Akipiga stori na paparazi wetu, Bozi alisema tatizo kubwa lililomkuta Nay kwa mpenzi wake Siwema kumfumania na njemba ni malipo ya kupuuza penzi lake na dhambi kubwa aliyomtendea ya kusambaza picha zake za utupu alizomtumia wakati walipokuwa kwenye uhusiano.
Emmanuel Elibariki ‘Nay’
“Nilimpenda mno Nay lakini fadhila ya penzi
langu akaona anidhalilishe kwa kuanika picha zangu za utupu kwenye
mitandao ya kijamii, jambo linalonisononesha mpaka kesho, naamini
yaliyomtokea ni laana yangu anayotembea nayo kwani bado sijamsamehe kwa
kitendo kile cha ajabu alichonifanyia,” alisema Bozi.
Post a Comment