ROSE NDAUKA: WALEMAVU WAMDONDOSHA CHOZI
STAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka hivi karibu
alijikuta akimwaga machozi baada ya kutembelea shule ya watoto wenye
ulemavu ya Salvition Army, iliyopo Kurasini jijini Dar.
Staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka.
Staa huyo akiwa na timu yake ya Rozzie Magazine, walibeba misaada
mbalimbali ikiwemo mchele, mafuta, maharage na sukari ambapo mara baada
ya kufika kwenye ukumbi maalum uliotaarishwa kwa ajili ya kuzungumza na
watoto hao, alishikwa na moyo wa huruma na kudondosha machozi.
Rose akiwa amebeba bidaa kwa ajili ya walemavu.
“Kuna kitu nimejifunza hata kama hatuna tunahitaji kuja kuonana na
watoto hawa kuzungumza nao na kuwafariji hivyo hata wasanii wenzangu
wanapaswa kufanya hivi kwani ni muhimu katika maisha yetu,” alisema
Rose.
Post a Comment