Petitman: Bora Ninyang'anywe Mke Kuliko Kuachana na Wema Sepetu
Mfanyakazi wa kampuni ya Endless Fame, Petitman ambaye mara zote ameonekana kuwa karibu sana na bosi wake , Wema Sepetu amesema kamwe hawezi kuacha kuwa karibu na Wema eti kwa sababu Wema na Diamond wameachana, ukizingatia kuwa Pititman na Diamond ni mtu na shemeji yake. (Petitman amemuoa dada yake Diamond, Esma)
Kauli hiyo inaashiria kwamba Petitman yupo tayari kunyang'anywa mke endapo uhusiano wake na Wema Sepetu hautaipendeza familia ya Diamond kuliko kuvunja uhusiano na Wema Sepetu ..
Petitman aliyasema hayo redioni alipoulizwa kama kuvunjiaka kwa mahusiano kati Wema na Diamond yana weza kutatiza ndoa yake na dada wa Diamond.
Alisema "Mimi na Wema ni Damu Damu ...ila mambo ya mahusiano kila mtu na mambo yake hatuingiliana wala…”.
Pititman na Wema kwasasa wanaonekana kuwa karibu zaidi na masanii Ommy Dimpoz ambapo wote wawili wameshiriki kwenye video ya wimbo mpya wa msanii huyo unokwenda kwa jina la Wanjera.
Post a Comment