Kitanzi, Kisu au Bastola - 10

ILIPOISHIA
“Unamjua yule msichana mpya?” alisema Madam Bernadeta kwa kunong’ona huku akiendelea kumshikashika Julieth.
“Namjua si yule anayeitwa Salima?”
Salima alishtuka baada ya kusikia jina lake likitajwa, akatega masikio yake ajue ni nini kilichokuwa kikitaka kuongelewa kuhusu yeye.
Songa Nayo...
“Unamwonaje mzuri eee?” aliongea Madam Bernadeta huku mikono yake ikiwa kifuani kwa Julieth.
“Usiniambie kama tayari umeshampenda ukaniacha mimi!” Julieth alijibu kwa hasira zilizochanganyika na wivu huku akijitoa mikononi mwa Madam Bernadeta na kuketi kitandani.
“Aaa...hapana siyo hivyo ni hivi, kesho atahamia chumbani kwa Diana, ninataka uwe naye karibu. Hakikisha anafuata kila kitu atakachotakiwa kukifanya. Kikubwa ninataka uwe rafiki yake. Mpeleleze na uniambie kila kitu atakachokuwa akikifanya wakati mimi sipo karibu naye.”
“Usijali, ni hilo tu?” aliuliza Julieth na kushusha pumzi ndefu kifua chake kikiyeyusha chuki nzito na wivu ulioanza kujijenga moyoni mwake baada ya kumsikia Madam Bernadeta akimtaja huyo msichana mpya mbele yake.
Akasimama na kuufungua mlango, taratibu akatoka nje ya chumba hicho kisha akaufunga kama ulivyokuwa awali na kutembea hatua kadhaa hadi chumbani kwake, bila kujua kama kuna watu walikuwa makini wakiwasikiliza kila kitu walichokuwa wakizungumza Mr. John Chakos na Salima.
Ni wazi kuwa Salima alikuwa msichana mzuri wa umbo na sura, kila mtu aliliona hilo. Kwa Julieth uzuri wa Salima ukawa kikwazo kikubwa kwa kuwa alianza kuhofia taji lake la urembo wa ‘Serenity’ kunyakuliwa na msichana huyo mpya. Siku zote yeye ndiye aliyeonekana msichana mrembo kuliko wote humo ndani. Uzuri wake uliifanya thamani na hadhi yake iwe juu zaidi ya wasichana wote ambao huuzwa ndani ya jengo hilo.
Kila mgeni muhimu alipoingia nchini Tanzania, Julieth ndiye aliyepewa kipaumbele kutembea naye kuliko msichana mwingine yeyote. Hivyo ujio wa msichana mrembo na mzuri zaidi yake ulikuwa kikwazo kwake, alihisi kila kitu alichokuwa akiringia kilikuwa mashakani kuchukuliwa na Salima; kuanzia wateja, hadhi, marafiki na mwisho kabisa, penzi la Madam Bernadeta. Julieth hakufikiria kuruhusu hayo yote yatokee, aliwaza kufanya kila atakachoweza kupambana na adui yake.
***
Muda wote huo Salima alikuwa akitafakari kitu gani kilichowapa haki wasichana hao wawili wapange kumbembeleza yeye. Alijiuliza kwa nini alikuwa akitakiwa kuhama chumba chake kesho asubuhi na kuhamia chumbani kwa msichana waliyemtaja kwa jina la Diana?
Akili yake haikuweza kufikiria sawasawa katika hali hiyo, alitaka kuwa huru kwa kutoka humo ndani kwanza na kurudi chumbani kwake kabla muda haujazidi kuyoyoma.
Kama vile paka mwizi, aliinua shingo yake na kumchungulia Madam Bernadeta ambaye alionekana kuanza kukolea usingizi mzito kwa uchovu mwingi wa yote waliyoyafanya dakika chache zilizopita na Julieth.
Wataalamu wa saikolojia husema kwamba mtu akiwa katika dakika arobaini za mwanzo za usingizi, mfumo wake wa fahamu huwa katika hali isiyoeleweka kiasi kwamba mtu huyo hawezi kuamka mwenyewe wala kuamshwa hata kama kungetokea kitu cha kushtusha kiasi gani.
Salima alijifunza kuhusu hilo sehemu fulani lakini hakujua ilikuwa wapi moja kwa moja. Akilenga kutumia mbinu hiyo alisimama na kunyata taratibu akikipita kitanda cha Madam Bernadeta aliyekuwa akijigeuza mara kwa mara na kuusogelea mlango.
Kama mahesabu yake yalikuwa sawa, Madam Bernadeta hata kama angejigeuza vipi asingeweza kuamka muda huo, lakini kama mahesabu yake yalikuwa na hitilafu basi siku hiyo ndiyo ingekuwa arobaini yake japo kuwa siku thelathini na tisa zilizopita hakuzitumia kuchunguza vitu vya watu kama ilivyokuwa siku hiyo.
“Mungu nisaidie,” Salima alijikuta akisema kimoyomoyo na kunyonga komeo la mlango kisha akafungua haraka akatoka nje na kushuka ghorofa hilo isiyomhusu ambapo moja kwa moja aliingia chumbani kwake na kujifungia huku akihema kwa nguvu.
***
Asubuhi ya siku iliyofuata Side alijua lazima atakuwa na la kujibu kwa mkewe Sonia, hasa kumueleza kuhusu kila kitu ambacho kilitokea usiku wa jana yake na kuhusu huyo mwendawazimu aliyemhifadhi siku nzima ndani ya chumba cha wageni kwenye nyumba yao.
Huku macho yake akimkazia Side, Sonia alichukua sahani kubwa ya matunda na kumsogezea Dedan ambaye alitazama ulaji wake kwanza na kuiga mfano kutoka kwa mwenyeji wake Side ambaye aliyazoa matunda hayo na kuyameza huku mbegu tu akizitema kama sehemu isiyofaa kuliwa ya tunda hilo la zabibu.
Kwa utamu wa matunda hayo Dedan alijikuta akimaliza sahani nzima na kutaka tena na tena jambo ambalo liliendelea kumfanya Sonia azidi kumkazia macho mumewe Side.
Ghafla alamu ya mlango ikalia. Sonia akakimbilia chumbani kwake na Side akamficha Dedan mahala kisha akaenda kufungua mlango.Kwa kuwa kuua kulikuwa ndani ya damu yake, Henry hakuona shida yoyote zaidi ya kufurahia amri hiyo. Tofauti na zamani, siku hiyo wala dhamira yake haimsuti juu ya damu za watu alizozimwaga kwa mikono yake. Alikuwa akizidi kuendelea kufanya ushetani wake kwa furaha kabisa kama vile kuua ilikuwa ni aina fulani ya mchezo.
Si kilio cha Sonia wala machozi ya Dedan yalimfanya awaonee huruma na kuwaachia mateka wake hao. Badala yake Henry alikuwa akiwaangalia na kucheka kila mara Sonia alipolia kwa uwoga baada ya kumgusagusa na mdomo wa bastola yake.
Henry alichagua sehemu nzuri mbali kabisa na makazi ya watu kiasi kwamba hakupata bugudha yoyote kuwahifadhi mateka wake. Sauti ya vilio vya kimyakimya ndivyo ambavyo vilisikika eneo hilo kutoka kwa Sonia ambaye huenda angepiga makelele kwa nguvu kama tu asingefungwa kwa kitambaa kizito mdomoni.
***
Side aliingia kila chumba ili kuhakikisha kama kweli mkewe Sonia hakuwemo ndani; kitu ambacho kilikuwa sahihi. Akawaza labda alikuwa nje mahali fulani. Labda aliondoka bila kuaga!
Alitafakari wazo hilo na kutolipa uzito kwani Sonia hakuwa na tabia ya kutoka nje, alikuwa ni mtu wa kukaa ndani muda wote akihofia kujulikana na watu. Hata mavazi yake yalikuwa ni yale yaliyomficha mwili mzima na kuacha macho tu.
Alipokuwa akitembea kuelekea mlango wa nyuma ambao ndiyo ulikuwa umefunguliwa, Side aligundua alama za viatu asivyovifahamu kwenye ardhi ya mlango wake. Ni wazi mtu asiyemjua aliingia na kutoka ndani ya nyumba yake.
Kama vile mchunguzi wa masuala ya uhalifu (forensic), Side alitafuta kila mahala alama yoyote itakayomdhihirishia alichokuwa akikiwaza, kuwa jambo lililotokea muda mfupi nyumbani kwake lilikuwa ni utekaji nyara na si vinginevyo.
Mara akagundua kuchunika kidogo kwa rangi kwenye kichuma cha loki ya mlango ulioachwa wazi jambo lililomfanya agundue kuwa mlango huo ulisukumwa kwa nguvu na aliyeingia ndani. Moyo wa Side ukaanza kudunda kwa kasi kiasi cha jasho jingi kumtoka kama vile mtu aliyechanganyikiwa.
Side alishindwa kutoa taarifa polisi wala sehemu yoyote ya usalama kwa kuwa alihofia kwa kufanya hivyo atamuanika Sonia mbele ya wabaya wake.
Kuna ule muda mtu huwa hafikirii chochote zaidi ya kuwa na hofu isiyokuwa na mfano, muda huo ulikuwa juu ya Side kwa siku hiyo akaanza kutetemeka kwa woga. Moyo wake mara ulifanya pah! Aliwakumbuka watoto wake mapacha ambao alizaa na mkewe Sonia wote walikuwa katika shule ya malezi ya awali kwa watoto ‘Msami Day Care.’
Kwa kasi ya ajabu Side alifika shuleni lakini jibu ni kwamba hawakuwepo hapo na walimu hawakujua wapi walipokwenda ingawa ushahidi wa watoto hao kuripoti shuleni asubuhi ulikuwepo.
Kwa uchungu Side alifumba macho yake kwa nguvu, machozi yakimtiririka mashavuni kama mtoto mdogo. Kitu alichokuwa akikitaka kujua zaidi ni nani aliyekuwa akimfanyia mambo yote hayo?
Akiwa mwenye kukosa matumaini, simu yake ya mkononi iliita kwa namba asiyoifahamu akaipokea na kusikiliza:
“Haloo Side, kama unamthamini mkeo na watoto wako rudi nyumbani kwako haraka sana, nina zawadi yako,” iliongea sauti ya mtu asiyemfahamu kwa kujiamini.
“Sema unataka shilingi ngapi nikupatie, naomba uniachie familia yangu,” alisema Side kwa pupa huku machozi yakimtoka.
“Usiwe kama mwanamke Side, inuka uje mara moja na nikukumbushe tu, uje peke yako ukifanya ujanja wowote mkono wangu sitauzuia juu ya watoto wako.”
“Nakuja naomba usiwafanyie jambo lolote baya.”
“Kuna usemi unaosema kuwa muuaji akilia hulia machozi ya kweli siyo bandia unajua maana yake? Ngoja nikwambie ni vile tu muuaji hujua maumivu ya mateso kuliko mtu yeyote yule, naamini unafahamu fika jinsi inavyokuwa. Una dakika kumi au nitaanza na mkeo,” alisema muuaji huyo na kukata simu.
Bila kupoteza muda, Side alikimbilia nyumbani kwake pasipo kujali hatari itakayomkuta.
***
Salima aliburuzwa mpaka ghorofa ya tatu, safari yake wakati huu ikaishia ndani ya chumba kimoja ambacho aliamini ndicho kilichokuwa kinakaliwa na msichana aliyesikia akizungumziwa usiku wa jana yake, Diana.
“Kuanzia leo hautaruhusiwa kukaa na simu wala kitu chochote kitakachokuwezesha kufanya mawasiliano nje ya jengo hili, mimi ndiye utakayepaswa kunisikiliza na kuniuliza kila kitu unachokiona haujakielewa. Sheria zetu zipo kila mahali ndani ya jengo hili kuwa makini uzisome kwanza kabla ya kufanya jambo lolote mahali popote, jambo la mwisho kuanzia leo jina lako litakuwa Carolina,” alimaliza kusema mwanamke huyo ambaye sauti yake, Salima aliikumbuka vyema kwa kuwa aliisikia jana yake.
“Huyu lazima atakuwa Madam Bernadeta,” aliwaza Salima masikio yake yakishindwa kuamini kama alipewa jina la mwanamke ambaye alikuwa hasimu wake wa muda mrefu kabla ya kuelewana naye dakika chache zilizopita.
Kwa kuwa kuua kulikuwa ndani ya damu yake, Henry hakuona shida yoyote zaidi ya kufurahia amri hiyo. Tofauti na zamani, siku hiyo wala dhamira yake haimsuti juu ya damu za watu alizozimwaga kwa mikono yake. Alikuwa akizidi kuendelea kufanya ushetani wake kwa furaha kabisa kama vile kuua ilikuwa ni aina fulani ya mchezo.

ITAENDELEA KESHO
Post a Comment