AMINA MWIDAU (VITI MAALUMU CUF) NDIYE MWENYEKITI MPYA WA KAMATI YA PAC
MBUNGE wa viti maalum Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF) ndiye
Mwenyekiti mpya wa Kamati ya PAC baada ya aliyekuwa mwenyekiti wake,
Zitto Kabwe kung'atuka kwenye nafasi yake ya ubunge.
Kupitia
akaunti yake ya Facebook, aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini
(Chadema) na Mwenyekiti wa Kamati ya PAC ambaye jana alijiunga rasmi na
Chama cha ACT-Tanzania, Zitto Kabwe amempongeza Amina kwa imani
aliyopewa na wajumbe wenzake wa Pac.
"Nimefanya kazi na Amina tangu mwaka 2010 tulipokuwa kamati ya POAC na nina imani, kwa ushirikiano mkubwa wa Makamu Mwenyekiti ndugu Deo Filikunjombe wataendeleza kazi tuliyoianza ya kujenga mfumo madhubuti wa Uwajibikaji nchini kwetu" aliandika Zitto Kabwe.

Post a Comment