ad

ad

VIJIMAMBO: OKWI, SSERUNKUMA WAFUNGIWA HOTELINI

Emmanuel Okwi.
WASHAMBULIAJI wa Simba, Emmanuel Okwi na Dan Sserunkuma wamefungiwa hotelini kutokana na deni.
Wachezaji hao akiwemo Joseph Owino, walijikuta katika tafrani na uongozi wa hoteli kutokana na kushindwa kulipa fedha ya malazi katika hoteli hiyo maarufu eneo la Sinza White Inn jijini Dar es Salaam.
“Hawa wachezaji walikuja kukaa hapa, ajabu hawajalipa hadi deni limefika shilingi milioni moja na laki sita.
 
Dan Sserunkuma.
Ajabu tumekuwa tukiona kuna dalili za kututoroka,” alisema mmoja wa wahusika katika hoteli hiyo.
“Tuliwasiliana na uongozi wa Simba ambao ulionyesha kushangazwa na wao kuwa hapa kwa kuwa uliwapangia hoteli nyingine. Hata hivyo tunaushukuru uongozi huo kwa kuonyesha uungwana na kukubali kutulipa.”
Viongozi wa Simba walionekana kutotaka kulizungumzia suala hilo walipotafutwa jana, lakini kiongozi mmoja wa kamati ya utendaji aliamua kufunguka.
“Unajua inashangaza, wachezaji hao walikataa nyumba waliyopewa. Hiyo nyumba alikuwa akiishi Tambwe na wachezaji wengine.
“Tukawapangia Sapphire Hotel ambayo ni moja ya hoteli bora kabisa. Wameondoka bila ya ruhusa na kuhamia (anaitaja hoteli).
“Nafikiri wanaonyesha wazi kuwa wao ni watovu wa nidhamu, hili si jambo zuri na linaweza kuupaka uongozi matope.”
Taarifa zinaeleza Okwi na wenzake wamekuwa wakiusumbua uongozi wa Simba mara kadhaa kwa kuomba ruhusa kila wakati au kupinga sehemu fulani waliyotakiwa kukaa.
Kwa sasa, Simon Sserunkuma yuko nchini Uganda, imeelezwa amekwenda kwenye 40 ya msiba wa mmoja wa wazazi wake.

No comments

Powered by Blogger.