MAJIBU YA JAY DEE NA GARDNER KUACHANA YAPO HAPA
BAADA ya wiki iliyopita aliyekuwa mke wa mtangazaji
wa kituo cha radio cha EFM, Gardner G Habash, mwanamuziki Judith
Wambura Mbibo ‘Lady Jay D’ kumwaga sababu za kuachana na mumewe huyo,
mkali huyo wa kutangaza ameibuka na kusema amechukizwa na maneno
yaliyotolewa na aliyekuwa mwandani wake huyo huku akidai anamuachia
Mungu.
Magazeti Pendwa kutoka Global Publishers yakaamua kumtafuta Gardner ili aweke bayana juu ya suala la ndoa yao kutokana na mwanamuziki huyo kuweka wazi kwamba tayari ndoa yao ilikwishasambaratika.
“Alichokisema na ulichokisikia ndiyo ukweli wenyewe. Hakuna ndoa tena, tumekwishaachana na kila mmoja kuchukua kilicho chake. Ila kila kitu namwachia Mungu na wala sina kinyongo naye,” alisema Gardner.
Akifunguka zaidi, Jide alisema kwamba alichoshwa na tabia hizo ambazo alipobanwa zaidi ili aziweke wazi tabia hizo, alisema kwamba mwanamume huyo alikuwa na tabia ya kuwashikashika wanawake kila alipokuwa jukwaani akiimba.
Alipenda kuwatongoza wanawake wengi tu ambapo kuna siku alimkuta akimshikashika mapaja mwanamke ndani ya mghahawa wake, na alipomuuliza, alikiri kufanya hivyo na kuomba msamaha.
Wawili hao walifunga ndoa Mei 14, 2005, jijini Dar es Salaam ambapo mpaka wanaachana, hawakubahatika kupata mtoto.
Gardner G Habash na Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jay D’ siku ya harusi yao.
Ishu hiyo iliyopata nafasi kwenye vyombo mbalimbali vya habari,
ilitokana na Jide kuwapa watu nafasi mashabiki wake kumuuliza maswali
katika mtandao wa kijamii, ambapo asilimia kubwa walitaka kujua kama
kweli ameachana na mume wake au la.Magazeti Pendwa kutoka Global Publishers yakaamua kumtafuta Gardner ili aweke bayana juu ya suala la ndoa yao kutokana na mwanamuziki huyo kuweka wazi kwamba tayari ndoa yao ilikwishasambaratika.
“Alichokisema na ulichokisikia ndiyo ukweli wenyewe. Hakuna ndoa tena, tumekwishaachana na kila mmoja kuchukua kilicho chake. Ila kila kitu namwachia Mungu na wala sina kinyongo naye,” alisema Gardner.
...Wakiwa kwenye pozi.
Siku chache zilizopita mwanamuziki Jide alifunguka kwamba hakutaka
tena kuendelea kuishi na mume wake kutokana na tabia mbaya alizokuwa
nazo mwanamume huyo, hali iliyomfanya kuishi pasipo kuwa na furaha
katika kipindi kirefu cha ndoa yao.Akifunguka zaidi, Jide alisema kwamba alichoshwa na tabia hizo ambazo alipobanwa zaidi ili aziweke wazi tabia hizo, alisema kwamba mwanamume huyo alikuwa na tabia ya kuwashikashika wanawake kila alipokuwa jukwaani akiimba.

Post a Comment