IDD AZZAN ASHTUSHWA KUPIGWA ZENGWE LA KUTOGOMBEA
Stori: OSCAR NDAUKA
KUMEKUCHA sasa! Mbunge wa Kinondoni kwa ‘leseni’ ya chama tawala (CCM), Idd Mohamed Azzan ameibuka na kusema kuwa ameshangazwa na habari zilizotangazwa na kituo kimoja cha runinga nchini kwamba amesema mwaka huu hataweka mguu wake kugombea ubunge wa jimbo hilo.
Akizungumza na Uwazi ‘Mizengwe ya Uchaguzi’ jijini Dar hivi karibuni, mheshimiwa Azzan alisema:
“Nimeshtushwa sana kusikia ikitangazwa kwamba eti mimi nimetangaza kutogombea ubunge Kinondoni mwaka huu. Nimesema lini na wapi na huyo mwandishi niliyemwambia ni nani?
“Hizi habari nahisi zimetengenezwa na maadui wangu kwa lengo la kuniharibia. Mimi sijasema sigombei, wananchi wa Kinondoni wanajua nini nafanya kwao na bado wananihitaji.”
Mheshimiwa huyo alikanyaga miguu kwa kwenda mbele zaidi akisema kuwa, mtangazaji aliyetangaza habari hiyo (jina lipo) alimpigia simu kumuuliza akajikanyaga lakini cha ajabu siku ya pili akatangaza tena kwenye redio ndugu na runinga hiyo kwamba alipigiwa simu na mheshimiwa kumuulizia kuhusu habari za yeye kutogombea.
“Sasa jamani kama uandishi wenu ni huo, kuweka hadharani mambo ambayo mhusika hajasema tutafika kweli?” alihoji Azzan na akasisitiza kuwa atagombea mwaka huu kama miaka mingine.
Uwazi Mizengwe: Unadhani zengwe umepigwa na nani mheshimiwa?
Azzan: Unajua huu ni mwaka wa uchaguzi, kwa hiyo maadui ni wengi sana na ndiyo wakati wao, nawajua lakini sitawataja.
Uwazi Mizengwe: Pole sana mheshimiwa.
Azzan: Ah! Bwana wee! Siasa zetu hizi!
Post a Comment