YANGA YAITULIZA SHABA 1-0, YAONDOKA NA POINTI 9 ZA MAKUNDI
Yanga imemaliza hatua ya makundi kwa kuwa na
pointi 9 baada ya kupata ushindi wa tatu mfululizo.
Yanga imeifunga Shaba kwa bao 1-0 katika
mechi ngumu katika michuano ya Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan,
Zanzibar.
Pamoja na kushambulia sana na kukosa sana,
Yanga walilazimika kusubiri hadi dakika ya 86 wakati Andrey Coutinho alipofunga
bao kwa kichwa akiunganisha krosi ya Simon Msuva.
Yanga walipoteza nafasi zaidi ya tano za wazi za kufunga kupitia kwa Mrisho Ngassa, Simon Msuva na Amissi Tambwe.
Post a Comment