SIKU ZA DIAMOND KUWA NA ZARI ZINAHESABIKA
WASWAHILI wanasema ngoma ikivuma sana hupasuka. Msemo huu unalandana na penzi la Zari ‘The Boss Lady’ na nyota wa muziki Afrika, Diamond Platnumz, baada ya mapenzi yao kuchukua sura mpya.
Licha ya vyombo vya habari Tanzania kuyapalilia mapenzi ya wawili hao, hali ni tofauti nchini Uganda ambako mapaparazi wamekuwa wakiibua mambo ya sirini ya msanii na mwanamama huyo tajiri nchini humo.
Kikubwa kinachozungumziwa ni kuhusu tabia ya Zari kutoka na wanaume tofauti. King Lawrence, anayedaiwa kuwa mpenzi wa Zari ametangaza dau la Dola 40,000 kwa Diamond ili amwache dada huyo.

Hakuishia hapo, alimwita Diamond majina mabaya, huku Zari akijibu katika mtandao wa Faceboo: “Ukweli ni kwamba watu wakijua una furaha wanaanza kukuharibia.”
Post a Comment