ad

ad

POLISI KUWAVAA SIMBA ROBO FAINALI, KOMBE LA MAPINDUZI



KCCA ya Uganda imevuliwa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi baada ya kufungwa na Polisi ya Zanzibar kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 Uwanja wa Amaan, Zanzibar. 
 

Polisi sasa itamenyana na Simba SC katika Nusu Fainali keshokutwa Uwanja wa Amaan, ambayo jana iliitoa Taifa ya Jang’ombe kwa mabao 4-0.
 

Kipa wa Polisi, Nasir Suleiman amepangua penalti mbili za Ivan Ntege na William Wadri, wakati Simon Namwanya aligongesha nguzo.
 

Waliofunga penalti za KCCA : Tom Masika, Ronnie Kiseka, Saka Mpiima na Owen Kasuule.
 

Waliofunga penalti za Polisi:  Daniel Justine, Mohammed Seif, Abdallah Mwalimu, Mohammed Salum na Ally Khalid, wakati waliokosa ni Suleiman Ali aliyepaisha na Juma Ali Silima ambayo ilipanguliwa na kipa wa KCCA, Yassin Mugabi.   
 

Polisi ambayo ilifungwa 4-0 na Yanga SC katika mchezo wa Kundi A, leo ilitumia mtindo wa kujihami zaidi mbele ya KCCA na hatimaye dhamira ikatimia kwa kuwavua ubingwa kwa penalti Waganda hao.

1 comment:

  1. My building manager from dove mountain real estate is a nice guy and helped me set up my bill pay! Few of us are single ladies and we all agree that he has gone above and beyond for building security recently.

    ReplyDelete

Powered by Blogger.