MANCHESTER CITY YALALA NYUMBANI, YACHAPWA 2-0 NA ARSENAL
KLABU ya Manchester City imepokea kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Arsenal ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wake wa Etihad jijini Manchester jana.
Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu ya England, mabao ya Arsenal yamewekwa kimiani na Santi Cazorla kwa penalti huku la pili likifungwa na Olivier Giroud kwa kichwa.
Kwa matokeo ya leo, Manchester City imeendelea kubaki nafasi ya pili ikiwa na pointi 47 huku ikiwa na pointi 5 nyuma ya vinara wa ligi hiyo, Chelsea wenye pointi 52. Asenal wapo nafasi ya tano wakiwa na pointi 39.
Post a Comment