ad

ad

LUIS FIGO KUGOMBEA URAIS FIFA

STAA wa zamani wa Ureno, Luis Figo jana Jumatano ametangaza kwamba amejikita kugombea nafasi ya kuwa rais wa Shirikisho la soka la kimataifa (Fifa) na kusisitiza kwamba vigezo anavyo.
 

Mwanasoka huyo wa zamani wa klabu za Real Madrid na Barcelona alisema kwamba ataingia vitani kupambana na Sepp Blatter kwa sababu anaamini soka inahitaji kupata hadhi bora zaidi tofauti na ilivyo kwa sasa.

Figo, 42, aliwahi kuchaguliwa kuwa Mwanasoka Bora wa Dunia mara mbili ameichezea Ureno mara 127 na kufunga mabao 32.

“Naujali sana mchezo wa soka na nikitazama taswira ya Fifa, si miaka ya karibuni bali tangu zamani kunaonekana kuwa na tatizo,” alisema.

Figo kwenye kinyang’anyiro hicho atashindana na Blatter, Prince Ali Bin Al-Hussein wa Jordan, Jerome Champagne wa Ufaransa, staa wa zamani wa Ufaransa, David Ginola na Rais wa Shirikisho la soka Uholanzi, Michael van Praag.

No comments

Powered by Blogger.