ad

ad

KITANDA CHA MAMA MWENYE NYUMBA - 08



ILIPOISHIA
”Abee bosi...”

”Hivi mzoa taka hakutoka kweli?”

”Mimi sina kumbukumbu nzuri bosi zaidi ya kumwona akiingia.”

”Kutoka hukumwona..?”

”Ukiwa jikoni si rahisi bosi kumwona.”

”Oke sawa, ndani hayupo. Oke kwaheri, lakini asante kwa ushirikiano wako.”

”Sawa bosi wangu.”

Baba Joy alirejea sebuleni akatoa kiti na kukaa nje ya nyumba eneo ambao hakuna mtu anayeweza kuingia ndani kwake kupitia getini nila yeye kumwona kwa macho...

”Chai taayri,” mkewe mama Joy alimwambia…

“Niletee hapahapa.”

Chai ilipelekwa pale nje, mama Joy moyoni alikuwa akichekelea kwani alijiona ni mshindi. Baada ya kumwekea chai mumewe aliingia ndani akaenda jikoni…

“Helena…”

“Abee bosi…”

“Mzoa taka alitoka?”

“Nilimtoa mama, si unasema mi mnafiki, lakini hebu ona wema niliyokutendea…”

“Ulimtoaje?”

“Mpaka getini…”

“Mlinzi hakumuona?”

“Ndiye aliyemfungulia mlango…”

“Akasemaje?”

“Alitaka kumkatalia asitoke ili baba amuone…”

“Sasa, ikawaje?”

“Nilimwambia afanye hivyo halafu mimi niseme hata yeye alipolala na wewe usiku wa juzi…”

“Una uhakika..?”

“Niliwaona mama…”

“Kelele…”

“Basi bosi…”

“Sasa sikia, hakikisha baba Joy hapati taarifa potofu kuhusu mimi na mzoa taka, akikuuliza simamia uongo, mwambie kwamba alikuja akazoa taka na kuondoka zake…”

“Lakini bosi…”

“Lakini nini sasa..?”

“Kuna kitu kimoja hujakijua…”

“Kama..?”

“Fuko la mzoa taka…”

“Limefanyaje?”

“Huna habari..?”

“Ningekuuliza Helena..?”

“Liko mlangoni nje pale…”

“Mh! Kweli..?”

“Hata sasa lipo…”

“Baba Joy ameliona..?”

“Amekaa nalo jirani, si amekaa nje..?”

”Ndiyo... lakini bado uongo utashika nafasi yake, utasema alichukua fuko jingine zuri alipewa na mama.”

”Si mzee atakasirika kutoa fuko jipya zuri kumpa mzoa taka asiyempenda..?”

”Afadhali uovu huo kuliko wa kitandani...”

”Sawa bosi.”



***

Mzoa taka alifika kijiweni akiwa anahema kwa kasi ya ajabu...

”Msela vipi?” msela mwenzake alimuuliza…

“Ni noma, nusu nidakwe…”

“Na nani?”

“Mwenye mji, ye kazuka tu bila mawasiliano na mkewe…”

“We ulikuwa wapi?”

“Si kwenye kitanda…”

“Cha nani..?”

“Cha mama mwenye nyumba, nikazama nikaibuka, nilipofika getini eti ulinzi shirikishi naye anataka kuniwekea wingu, ningemtoa roho ujue, mi sioni noma kulala jela, maisha yenyewe nimeshachoka nayo.”



***

Baba Joy baada ya kumaliza kunywa chai, alimuita mlinzi wake, Fuko…

“Hebu vuta kiti ukae hapa nataka kusema na wewe…”

“Sawa bosi.”

Baada ya mlinzi kukaa, baba Joy alimwangalia kwa macho makubwa kisha akachukia…

“Huu mfuko mchafu ni wa nani..?”

”Mzoa taka bosi...”

”Yuko wapi..?”

”Sijajua bosi...”

”Una maana gani..?”



”Nina maana sijajua aliko kwa sasa...”

“Mimi nahisi kazi imekushinda…”

“Hapana bosi, haijanishinda…”

“Sasa kwanini usijue nani kaingia nani katoka wakati we upo getini...?”

“Nisamehe bosi…”

“Sasa sikia, ili uendelee kuwa kazini nijibu swali langu moja tu…”

“Sawa bosi…”

“Mzoa taka alipoingia alipitia wapi?”

“Pale getini bosi…”

“Alitoka..?”

“Sijamuona bosi…”

”Sasa nakupa kazi, mimi nitaangalia geti, wewe nenda ndani, zunguka kote hakikisha unampata mzoa taka kisha mlete hapa kwangu, sawa?”

”Sawa bosi.”

Mlinzi Fuko alikwenda ndani, alianza kwa kufikia jikoni ambako alimkuta Helena...

”Leo balaa,” alianza kwa kusema...

”Balaa kivipi?”

”Sai bosi...”

”Bosi gani..?”

”Mwanaume...”

”Kafanyaje?”

”Mh! Eti kaniambia niingie huku ndani, nimtafute mzoa taka kila sehemi hadi nimpate kisha nimpeleke kwake...”

”Ah! Hilo tu...”

”Unasema hilo tu sasa nitampataje?”

”We zuga huku wee, kisha nenda kamwambie hujamuona, unahisi ulipokuwa ndani yeye katumia mwanya huo kutoka getini...”

”Mh! Unajua yeye yuko wapi?”

”Si sebuleni..?”

”Nani kasema, amekaa getini. Kasema anashika nafasi yangu ili mtu asiingie wala kutoka.”

Mara, mama Joy alitokea jikoni...

”Fuko unafanyaje hapa..?”

”Bosi kuna tatizo kubwa...”

”Ni tatizo gani linakufanya uache lindo na kuja kukaa hapa, geti unamwachia nani?”

”Getini yuko bosi...”

”Yuko bosi! Una maanisha baba Joy..?”

”Ndiyo bosi...”

”Kwanini..?”

”Aliniita, akaniuliza kama nilimwona mzoa taka akiingia, nikamjibu ndiyo, akaniuliza nilimwona akitoka? Nikamjibu sijamwona, ndiyo akasema nimtafute humu ndani hadi nimpate, yeye amekaa getini kuchukua nafasi yangu.”

Mama Joy alivuta pumzi, akawa mambo mengi. Aliwaza kuwa, mlinzi wake alikuwa sahihi au si sahihi kumjibu mumewe kwamba, mzoa taka aliingia...

”Lakini si alishajua aliingia, sasa labda kwenye kutoka, angemjibuje, alimuona akitoka au hajamuona...?”

”Oke, wewe rudi, mwambie Helena amekwambia mlinzi alitoka...”

”Hapana bosi, hata mimi nilimwambia sijamwona akitoka...”

”Alikuuliza saa ngapi?”

”Muda si mrefu bosi...”

”Alikuja jikoni..?”

”Ndiyo bosi.”

”Mh! Baba Joy naye kwa kubana...”

”Ni kweli bosi, amekubana sana, huna ujanja,” alisema mlinzi huku akicheka hali iliyomkera sana mama Joy...

”Kwako ni furaha na amani au?” mama Joy alimuuliza Fuko...

”Hapana bosi, unajua mzee amechezwa na machale na inabidi utengeneze sana ili asiendelee kukuchunguza, ni hatari kwako...”

”Umeyatoa wapi maneno hayo..?”

”Ni mawazo yangu tu bosi...teh! Teh! Teh!”

Mama Joy alitoka kwa kasi na kwenda chumbani kwake. Kule nyuma, Helena na Fuko walijiuliza...

”Sasa bosi anapoondoka na hasira anategemea nini? Yeye ndiyo alitakiwa kushauri nini kifanyike ili kuondoa hii hali,” alisema Fuko...

”Sasa ndiyo imetokea wewe tafuta njia...”

”Sina njia, labda nisaidie wazo.”

Helena alitulia kwa muda kisha akasema...

”Sikia, mfuate bosi getini, mwambie umekagua kila mahali hujamwona mzoa taka. Lakini una wasiwasi na chumbani kwake maana ni huko tu ndiko hujafika...”

”Mh! Je, kama na yeye akienda na kukagua kila mahali huko chumbani, hata chini ya kitanda, kabatini, chooni, bafuni kote asipomwona mzoa taka si atajua amepita getini..?”

”Mwambie kuna wakati mama alikutuma dawa ya meno, labda alitumia muda huo wa kukutuma kumtoa mzoa taka...”

”Eee, sawasawa, hapo nakubaliana na wewe,” alisema mlinzi na kutoka jikoni. Alirudi getini...

”Yuko wapi mzoa taka, fuko lake chafu bado liko hapa na wewe nimekwambia lazima umlete kwangu,” baba Joy alisema...

”Bosi, nimemsaka kila mahali lakini wapi! Nina wasiwasi na chumbani kwako kwa sababu ndiko mahali pekee sijafika...”

”Chumbani nilimtafuta hadi ndani ya kabati la nguo, hayupo. Bado kesi iko kwako. Lazima alipita hapa getini, je alipitaje?”

”Ee bosi nina wasiwasi na jambo moja...”

”Lipi hilo..?”

”Labda alipita wakati bosi mdogo aliponituma dawa ya meno dukani.”

”Alikutuma dawa ya meno?”

”Ndiyo bosi...”

”Ulitumia dakika ngapi kwenda na kurudi?”

”Kama kumi bosi, maduka ya kule chini karibu na barabara.”

Baba Joy alitingisha kichwa kama kukubaliana na maneno ya Fuko...

”Oke...sawa, ni nimekuelewa vizuri, endelea na kazi,” alisema baba  Joy.

Alisimama mlango mkubwa na kumwita mkewe...

”Mama Joy...”

”Abee.”

Sekunde kadhaa mbele, mama Joy alisimama mbele ya mumewe...

”Abee...”
”Hili fuko la taka hapa chafuchafu vipi?”

Mama Joy hakujibu kitu, alilifuata, akainama kuliokota na kuondoka nalo. Wakati anaondoka, baba Joy alimtupia macho mwanzo mwisho, akabetua vidole na kuzama ndani.



***

Asubuhi iliyofuata, baba Joy aliondoka kwenda ofisini kwake kama kawaida. Alikuwa na ahadi za kibiashara kama tano baada ya kuwa Arusha.

Nyuma, mama Joy alioga, akajipodoa vizuri sana na kutoka hadi getini...

”Fungua geti,” alimwamuru Fuko...

”Sawa bosi,” mlinzi alifungua geti kwa wasiwasi huku akikumbuka alivyomchongea mwanamke huyo kwa mumewe jana yake kwamba anahisi alimtoa mzoa taka jana yake alipomtuma dukanu kununua dawa ya mswaki.

Baada ya geti kuwa wazi, mama Joy alitoka nje na kusimama akiangaza kulia na kushoto...

”Sijui kijana wangu mzoa taka atakuja au ndiyo ameingiwa na woga? Angekuja japo nimwone kwa macho tu...nakapenda katoto kale...kanayajua mambo.”

***

Baada tu ya kufika ofisini, baba Joy alimuuliza sekretari wake mambo mawili matatu kama yalitokea wakati amekwenda Arusha...

”Yule mzungu wa Adams Company alikuja, pia wale Wahindi wa Singapore wamefika jana, watakuja leo. Mambo mengine bosi yapo kwenye infile zako bosi...”

”Oke,” baba Joy alipitiliza hadi mezani kwake, ila anakaa tu akakumbuka kitu...

”Hivi, yule Fuko aliniambia kuhusu kununua dawa ya meno, wakati napiga mswaki asubuhi ile dawa ilikuwa mpya au ya zamani? Mbona kama sikumbuki kitu chochote pale,” alisema moyoni baba Joy.

Alisita kwanza kufanya jambo lolote lile na kuwaza kuhusu hilo la dawa ya meno...

”Noo! Pale hapakuwa na dawa mpya, ingawa sina uhakika na hili, oke, nitalifanyia kazi.
ITAENDELEA SIKU YA KESHO

No comments

Powered by Blogger.