ad

ad

KITANDA CHA MAMA MWENYE NYUMBA - 07




ILIPOISHIA
“Ngo ngo ngooo,” geti kubwa liligongwa…

“Labda huyo…”

“Hebu fungua.”

Fuko alifungua geti, macho ya mama Joy yalikuwa makini kutaka kujua ni nani anaingia maana nyumba yake huingia watu wengi…

“Shikamoo mama,” alikuwa mzoa taka bwana!

Siku hiyo alilipuka kwa suruali ya ‘jinsi’ ya mtumba na t-shirt pia ya mtumba iliyoandikwa kifuani I AM NO BODY! Nguo zote hizo alitokelezea nazo bila kuzifua. Ile 50,000 aliyohongwa na mama Joy jana yake ndiyo alifanyia shoping hiyo.

Mama Joy alianza kwa kuachia tabasamu kabla ya kuitikia shikamoo hiyo, alimkazia macho mzoa take…

“Kofu…”

“Naam mama,” mzoa taka aliitika akiwa ameshika fuko mkononi…

“Umependeza sana leo baba…”

“Asante mama.”

Kifupi, mama Joy alitokea kumpenda sana mzoa taka kuliko mlinzi kwa sababu moja kuu. Mzoa taka alikuwa akimbeba mpaka juu ya mlima wakati mlinzi kila alipokuwa akikaribia mlima alishidwa na kurudi nyuma.

Mama Joy alimshika mkono mzoa taka na kwenda naye ndani, sebuleni lakini alipofika mlangoni, mzoa taka huyo aliweka pembeni fuko lake…

“Hebu njoo wewe,” alimuita mfanyakazi wake…

“Hujambo kijana?” mfanyakazi alimsalimia mzoa taka.

“Sijambo, shikamoo.”

“Marahaba…”

“Hebu mpe huyu juisi au maziwa ya moto kama yapo.”



***

Baba Joy alikuwa akipita Mizani ya Kihaba, meseji ya Helena ilipoingia kwenye simu yake…

“Mwenzio mzoa taka ameingia sasa.”

Baba Joy alisukuma mafuta kwa kasi ya ajabu, baadhi ya magari yaliyokuwa yakitoka kwa mbele yake yalipisha pembeni yakiamini kuna tatizo.

Ndani ya dakika ishirini tu, baba Joy alifika nje ya geti la jumba lake la kifahari, akasimama huku mlinzi akiwa hajui kama bosi wake yuko nje. Alimtumia meseji Helena…

“Bado yumo ndani?”

“Yumo. Walikuwa sebuleni, sasa wameenda chumbani kwako wenzio. Da! Mzoa taka bosi yupo kwenye kitanda cha mama mwenye nyumba. We ukifika Dar njoo hadi nyumbani kwako.”

Baba Joy alitamani kupaa. Hakutaka kupiga honi ili afunguliwe geti, akafungua mlango na kushuka.

Alipofika getini alilisukuma. Kwa bahati njema, baada ya mzoa taka kuingia, mlinzi alisahau kulifunga geti hilo kama ilivyo kawaida yake…

“Ha! Shikamoo bosi…mi sihusiki lakini. Halafu tulimwambia mama hakutusikia,” alisema mlinzi.

Baba Joy alimpuuza na kutembea kwa kasi kwenda ndani. Hakushuka na brifkesi wala kitu chochote kile kingine.

Alipofika kwenye mlango mkubwa alishtuka kwanza kwa kuona fuko chafuchafu la mzoa taka.

“Huyu mwanaharamu leo namtoa ubongo, ndiyo dawa pekee,” baba Joy alisema moyoni akiwa sebuleni sasa. Akakumbuka kuwa, aliposhuka alisahau bastola kwenye gari lake, akairudia.

Mlinzi alishangaa sana kumwona bosi wake akitoka mbio…

“Kuna nini bosi, mbona unakimbia hivyo?”

“Shii,” baba Joy alimkataza mlinzi kwa kuweka kidole kwenye midomo.

Sauti ya mlinzi ilimfikia mama Joy kule chumbani, akashtuka kidogo...

“Mh!” aliguna…

“Vipi?” mzoa taka alimuuliza…

“Mlinzi wangu sijui anaongea na nani?”

“Si kuna mama mwingine anafanya kazi ndani kwako…”

“Ee, labda huyo.”

Kwa bahati mbaya sana, mama Joy aliisikia sauti ya mlinzi wake lakini hakujua alichokuwa akikiongea. Aliachana na mambo ya nje kwa mlinzi na kumgeukia mzoa taka…

“Baby wangu, leo itakuwa kama jana..?”

“Kuhusu nini..?”

“Mambo yetu…”

“Yapi..?”

“Aaah! Nataka tukimalizana mimi na wewe nisimfikirie mwanaume mwingine tena leo.”

“Wewe tu, mimi mbona niko poa wangu.”

Mama Joy alimshika mzoa taka, akamvutia kwake na kumuomba denda kwa ishara. Lakini ghafla machale kama yalimcheza, alichukua simu ya mezani na kupiga getini…

“Halo getini hapa, Fuko naongea…”

“Nimesikia sauti yako ja juu sana, ulikuwa unaongea na nani?”

“Siyo mimi mama,” mlinzi alijibu…

“Una uhakika..?”

“Ndiyo bosi.”

Mama Joy akakata simu.



***

Baba Joy alisukuma geti, akazama akiwa na bastola mkononi…

“Ili aniheshimu lazima nimbandue jicho la kushoto,” alisema moyoni baba Joy.



***

Mama Joy na mzoa taka wake, walizama katika denda kiasi kwamba, walikuwa wakichuruzisha mate. Muhemko wa mama Joy ndiyo uliosababisha mzoa take asimcheleweshe, akamshika na kumpindulia kitandani sasa…

“Waooo,” alisema mama Joy akijifanya anasikia raha.



***

Baba Joy alijiuma kidole akakunja uso. Alikumbuka mlango wa gari haukufungwa na ndani mlikuwa na fedha nyingi sana zikiwa waziwazi, akageuza na kutoka.

Wakati anatoma alibamiza mlango mkubwa wa sebuleni hali iliyomfanya mkewe, mama Joy agundue kuwa kuna mtu ama ameingia sebuleni kwake au ametoka.

“Na lazima mtu huyo atakuwa si mlinzi, maana mlinzi hawezi kuingia sebuleni kwangu bila ya ruksa,” alisema moyoni mama Joy, akatoka kitandani, akachukua khanga na kujifunga maana tayari alishavua nguo na kubaki kama alivyoingia duniani kwa mara ya kwanza…

“Kama ni mlinzi leo atanitambua. Ina maana kuwa na yeye kwa siku moja tu ndiyo ameshapata tiketi ya kufanya anavyotaka?”

Alipofika sebuleni, alishtuka kumwona mume wake akiingia getini tena akiwa kasi…

“Ooh! Mungu wangu nimekwisha mimi,” alisema mama Joy na kukimbilia chumbani. Alimkusanya mzoa taka na nguo zake na kumvuta kutoka naye hadi jikoni ambako mfanyakazi alikuwepo akiendelea na shughuli zake.

Mfanyakazi huyo alijifanya ameshtuka sana kuliona tukio hilo, lakini alikuwa analijua litakuwepo tu.

Mama Joy baada ya kumtelekeza mzoa take jikoni alirudi chumbani haraka, akaweka shuka vizuri na kujifanya amekaa.

Mlango ulisikumwa kwa nguvu, baba Joy akazama ndani huku akihema kwa kasi ya ajabu…

“Yuko wapi?” ndiyo swali alilomuanza nalo mkewe…

“Yuko wapi nani?”

“Huyo mzoa taka wako…”

“Mzoa taka wangu! Yupi huyo?” mama Joy alijibalaguza ingawa ukweli alikuwa akiujua. Alikuwa akitetemeka maana mumewe alishika bastola.



***

Kule jikoni, Helena alihisi mambo yataharibika zaidi kwa ndoa ya mabosi wake, alichofanya, alimchukua mzoa taka kumpeleka nje kwa njia ya uani.

Mlinzi getini alitaka kulipua bomu, lakini Helena akamuwahi…

“Unataka kusema nini, wewe je, hujawahi kulala kwa mama? Sema na mimi nikusemee.”

Mzoa taka alipitishwa, akasepa zake akiacha lile fuko chafu la takataka.



***

“Mimi si mwendawazimu eti niulizie nani halafu pasiwepo mtu, nina ushahidi wote kwamba yupo,” alisema baba Joy huku akiinama kwa lengo la kuchungulia chini ya kitanda…

Mama Joy alibaki kimya kwani aliamini kuingiza maneno mengi kusha aende akamnase jikoni angewamaliza wote, hata yeye.

Baba Joy alipoona mvunguni mwa kitanda hola, alilifuata kabati la nguo, akafungua humo, lakini hamkuwa na kitu, akaenda chooni ambako pia hakuona kitu.

Alitoka kwa hasira akimwacha mkewe chumbani hadi jikoni, hola. Akaenda kwenye vyumba vinne vya wageni, hamna kitu. Akenda chumbani kwa mfanyakazi…

“Si kawaida yangu kuingia humu lakini leo nimelazimika,” alisema baba Joy akitoka. Aliamua kwenda uani kwa nyuma ambapo ili afike huko lazima apitie jikoni, akakutana na Helena akiwa anaingia kutoka kumsindikiza mzoa taka…

“Hujambo..?”

“Sijambo bosi, habari za safari..?”

“Nzuri, mbona sijamwona..?”

“Hayupo ndani..?”

“Sijamwona, nimekuja hadi chumbani kwako lakini hamna kitu.”

“Kha! Atakuwa amekwenda wapi sasa? Aliingia naye lakini.”

“Au uliona vibaya, si ajabu aliingia kuzoa taka na kuondoka zake. Lakini hapana, huyu atakuwemo humuhumu ndani maana mlangoni nimekuta fuko lake chafu, linanuka,” alikandia baba Joy huku akitoka uani ambako pia hakufanikiwa kumwona mzoa taka. Hapo, bado mkononi alishika bastola yake tayari kwa kumtegua shingo mwizi wake.

Baba Joy alikwenda hedi getini…

“Fuko…”

“Yes boss…”

“Kuna mtu katoka baada ya mimi kuingia..?”

“Muda huu..?”

“Ndiyo muda huu…”

“Unataka kusema nini, wewe je, hujawahi kulala kwa mama? Sema na mimi nikusemee.”

Mlinzi alipokumbuka maneno hayo ya Helena, alijikuta akifunga kinywa chake…

“Sijaona mtu bosi…”

“Una uhakika..?”

“Kabisa kabisa bosi wangu…”

“Sasa funga geti, usifungue mtu kuingia wala kutoka hadi nitakaposema mimi.”

”Sawa bosi,” alisema Fuko kwa utii wote huku akimwangalia baba Joy kwa macho ya kuibia. Kama baba Joy angekuwa makini angegundua jambo geni kwenye macho ya Fuko…

“Nikisikia amepita mtu hapa mimi na wewe wewe na mimi.”

“Hapiti mtu bosi, si kuingia si kutoka.”

Baba Joy alikwenda ndani, alikagua kila sehemu ambayo aliamini inaweza kuwa na maficho ya mtu lakini hakuweza kumwona mzoa taka wala muokota makopo.

Alikwenda kwenye ukuta pembeni kabisa kisha akampigia simu Helana.

”Haloo bosi...”

”Helena...”

”Abee bosi...”

”Hivi mzoa taka hakutoka kweli?”

”Mimi sina kumbukumbu nzuri bosi zaidi ya kumwona akiingia.”


ITAENDELEA SIKU YA KESHO

No comments

Powered by Blogger.