KARDASHIAN AAJIRI MTAALAM AMPUNGUZE KILO SABA ALIZOONGEZEKA
Mtaalam huyo ameajiriwa ili amfundishe jinsi ya kupika chakula bora zaidi kwa ajili ya familia hiyo akiwemo mtoto wake wa kike mwenye umri wa miezi 19 aitwaye North.
Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 34 na mke wa mwanamuziki maarufu Kanye West, alisema: “Nimeanza kutafuta mtaalam wa mambo ya chakula kwani ninakula bila mpango. Nimeanza kula chakula bora na kufanya mazoezi ili kubadili mtindo wa maisha yangu hususan sasa ambapo nina mtoto. Ninataka kujua nini cha kupika na jinsi ya kupika chakula bora.”
Alipoulizwa iwapo anapanga kupata mtoto wa pili, alisema: “Ninatarajia jambo hilo. Tunajaribu na tunaombea jambo hilo litokee. Hivi sasa sina ujauzito lakini hivi sasa nimeongezeka kilo 15.”
Post a Comment