TAMBWE ATEMWA RASMI SIMBA NI AIBU KWA SIMBA!
MASTAA wa kimataifa wa Simba, Warundi, Amissi Tambwe na Pierre Kwizera, wameachwa rasmi na nafasi zao kuchukuliwa na Waganda, Juuko Murshid na Simon Sserunkuma ambao jana wamesaini mkataba wa miaka mitatu-mitatu.
Tambwe ambaye msimu uliopita, alitwaa kiatu cha mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara akifunga jumla ya mabao 19, amekuwa akihusishwa na tetesi za kuachwa tangu kufunguliwa kwa dirisha dogo, lakini mwisho wa siku jana ilibainika rasmi ametemwa.
Akizungumza Tambwe alifunguka kila kitu kuhusu sakata hilo na kusema kuwa alipewa taarifa hizo juzi Jumamosi baada ya mechi ya Nani Mtani Jembe dhidi ya Yanga SC.
Mganda, Simon Sserunkuma.
“Nimepewa taarifa, mimi na mwenzangu (Pierre), kwa hiyo tunajiandaa kuondoka kwenda nyumbani Burundi, ila kesho (leo) tutakwenda kuonana na viongozi wa Simba kwa ajili ya kutupa stahiki zetu, hivyo kufikia Ijumaa wiki hii tunaweza kuwa tumeondoka,” alisema nyota huyo wa zamani wa Vital’ O.
Hata hivyo, aliongeza kuwa kabla ya kupewa tamko hilo, Simba ilitaka kuwatoa kwa mkopo kwenda Mbeya City lakini hawakuwa tayari kwa kile alichosema wao si ‘levo’ ya wachezaji wa kutolewa kwa mkopo.
“Hatukuwa tayari kwenda kwa mkopo, sisi siyo watu wa aina hiyo, hivyo tumeona twende nyumbani tukapumzishe akili, kisha tutafute maisha kwingine,” alisema Tambwe huku akiongeza kuwa ni bora kwenda bure kuliko kucheza kwa mkopo.
Post a Comment