MATATIZO YA UZAZI KWA AKINA MAMA
Akina mama wana matatizo mengi, mojawapo kubwa linalowasumbua ni tatizo la kutokushika ujauzito.
Mwanamke kushindwa kupata ujauzito kwa kipindi cha ndani ya mwaka mmoja au zaidi ya mwaka mmoja wakati mwanaume na mwanamke wanakutana kwa muda unaotakiwa na bila kutumia njia za kuzuia mimba ni tatizo.
Kuna aina mbili ya tatizo hili moja hujulikana zaidi kwa jina la primary infertility. Hii humaanisha kuwa mwanamke hajawahi kushika ujauzito maishani mwake.
Pili ni secondary infertility, hii humaanisha kuwa aliwahi kupata mimba lakini ikashindikana kupata nyingine, na ya tatu ambayo hutokea mara chache kama asilimia 20 hujulikana kama fecundability ambapo mwanamke anakuwa na uwezekano wa kupata mimba ndani ya mzunguko mmoja wa hedhi.
Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 80 ya wanandoa hupata ujauzito bila ya kuwa na tatizo lolote kutokana na matakwa yao ambapo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wakiwa wanakutana mara kwa mara kimwili kati ya mara nne hadi tano kwa wiki na bila kutumia kinga basi huweza kupata ujauzito bila tatizo lolote.
Asilimia 10 ya wanandoa huweza kufanikiwa kupata mimba kwa kipindi cha miaka miwili ndani ya ndoa na asilimia 10 zilizobaki haiwezekani kabisa kushika ujauzito kwa kipindi cha zaidi ya miaka 2 ndani ya ndoa bila kutumia njia ya kuzuia ujauzito.
Vichocheo vinavyosababisha kutunga kwa mimba vipo vingi kama vile afya ya mbegu za mwanaume kuwa na uwezo wa kukimbia sehemu za juu ukeni karibu na shingo ya kizazi pia mbegu za mwanaume ni lazima zibadilike na ziweze kuogelea haraka kupitia kwenye shingo ya kizazi.
Lazima kuwepo na upevushaji wa mayai na mirija ili iwe na afya njema na isiwe na tatizo la kusafirisha yai.Mbegu ziwe na uwezo wa kuungana na yai na kusafiri kutoka kwenye mirija kwenda mji wa mimba na yai lililoungana na mbegu lazima lisafiri kwa muda wa siku nne hadi tano ili lifike kwenye mji wa mimba
Itaendelea wiki ijayo.
Post a Comment