KITAMBI KINAVYOWEZA KUSABABISHA MAGONJWA
Kitambi ni hali ya mtu kuwa mnene na tumbo kuchomoza ambapo mafuta ya ziada mwilini huongezeka eneo hilo kwa kiasi kikubwa. Mtu akiwa na kitambi anapata athari kubwa kama tutakavyoona.Hata hivyo, tatizo la kitambi kiafya linarekebishika.
Zamani hata sasa baadhi ya watu wanaamini kuwa mtu akiwa na kitambi basi hali yake kiuchumi ni nzuri au ni tajiri.
Watu wengi, wamekuzwa kwa kula chipsi-mayai, mikate na vyakula vya sukari na si mboga za majani na matunda.
Mbaya zaidi ni kwamba licha ya watu wengi kutofanya mazoezi ya kutosha kama ilivyokuwa zamani, watu wenye vitambi wanaonge zeka kila sehemu.
Ongezeko la tatizo hili la kiafya katika nchi nyingi linatisha. Kwa ujumla, umri wa mtu mnene mwenye kitambi huwa pungufu kwa miaka 8 had 10 ukilinganisha na mtu mwenye umbo la kawaida.
MAGONJWA
Hii inatokana na ukweli kwamba uzito wa mtu husababisha magonjwa ya moyo, aina fulani ya kisukari, magonjwa ambayo huua mamilioni ya watu duniani kote. Unene unaweza kusababisha moyo ukazungukwa na mafuta na kusababisha matatizo au ugonjwa wa moyo.
Lakini pia Ini linaweza kuzungukwa mafuta na kuleta madhara. Hata hivyo ini linaweza kuwa na mafuta mengi kutokana na unywaji wa pombe kupita kiasi. Mada hiyo tutaijadili kirefu katika matoleo yetu yajayo.
USHAURI
Kila mtu aepuke kula vyakula vyenye mafuta mengi na kutokula chakula kupindukia na ule unaposikia njaa, kutotia mafuta mengi kwenye chakula na kutotumia sukari nyingi.
Kila mtu anatakiwa kufanya mazoezi ya kukimbia, kutembea au kuogelea angalau kwa nusu saa kila siku.
Watu wanashauriwa kuacha kutumia vyakula vya kopo na hasa vile vyenye gesi nyingi. Wale ambao ni wanene kupita kiasi waonane na daktari kwa ushauri wa kitaalamu.
Mafuta kwenye ini
Unene husababisha matatizo kwenye magoti, figo na kwenye maini, leo tuangalie tatizo la kwenye ini.
Ugonjwa wa ini kuwa na mafuta (FLD), ni tatizo linaloweza kugeuzwa ambapo vipande vikubwa vya aina maalum ya mafuta ya trigliseride hukusanyika katika seli za ini kupitia mchakato wa steatosisi (yaani uwekaji usio wa kawaida wa mafuta ndani ya seli).
Itaendelea wiki ijayo.
Post a Comment