ad

ad

HANS PLUIJM ALETA FOMESHENI NNE YANGA


KOCHA wa Yanga, Hans Pluijm ametamba kutumia fomesheni nne zitakazompa ushindi katika mechi mbalimbali zijazo za timu yake.

Kocha huyo raia wa Uholanzi ambaye ana wiki moja tu tangu alipoanza jukumu la kuinoa timu hiyo, akiwa na msaidizi wake, Charles Mkwasa amejinadi kuwa amepanga kuanza na mifumo miwili kwenye mechi dhidi ya Azam FC, keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Pluijm ameweka wazi kuwa mifumo hiyo atakayoanza nayo keshokutwa ni 4-4-2 na 4-3-3 kabla ya kubadili na kuanza kutumia mingine ukiwemo ule wa 4-5-1.“Nisingependa kuweka wazi mifumo niliyopanga kuitumia kwenye mechi zetu kwa hofu ya wapinzani wetu, lakini nimepanga kutumia mifumo minne tofauti katika ligi na mashindano mengine.

“Mifumo hiyo nimepanga kuitumia kutokana na aina ya timu ninayokutana nayo kwenye mechi husika. Nitaanza na 4-4-2 na 4-3-3, nikiona mfumo mmoja ni mgumu basi nitabadilisha na kutumia mwingine,” alisema Pluijm.
Wakati huohuo, kocha huyo ameweka wazi kuwa Deogratius Munishi ‘Dida’ ataendelea kuwa kipa chaguo la kwanza kikosini hapo kutokana na uwezo ambao amekuwa kionyesha karika mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini.
Hivyo Dida atakuwa namba moja huku chaguo la pili akiwa ni Ali Mustapha ‘Barthez’ akifuatiwa na Alphonce Majogo aliyetua klabuni hapo hivi karibuni akitokea Friends Rangers inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.
CHANZO: CHAMPIONI

No comments

Powered by Blogger.