ad

ad

‘MADEREVA VIJANA HAWAPENDI KUFUNGA MIKANDA’



IMEBAINIKA kuwa idadi kubwa ya waendesha magari vijana hawafungi mikanda hivyo kuwafanya kuwa waathirika wakubwa wa ajali za barabarani ambazo zingeweza kuepukika.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Carmudi kanda ya Afrika ya Mashariki, William Day, alipozungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuhusiana na utafiti uliofanywa na kampuni yake inayojihusisha na biashara ya magari kwa njia ya mtandao.

Alisema tafiti zinaonyesha kuwa kitendo cha kufunga mkanda wakati wa kuendesha magari, kunaweza kupunguza idadi ya vifo vinavyosababishwa na ajali barabarani na hivyo kulinda nguvu kazi ya taifa.

Pia, tafiti zimeonyesha kuwa abiria waliokaa kiti cha mbele wanaweza kuepuka madhara kwa zaidi ya asilimia 45 zaidi ya asilimia 50 ya wale wa viti vya nyuma.
Day, alisema utafiti huo umebaini vile vile usomaji wa ujumbe wa simu, unywaji wa pombe uliopitiliza na hali mbaya ya magari ni kati ya sababu zinazosabisha idadi kubwa ya ajali ambazo zingeweza kuepukika kama sheria zilizowekwa zingefuatwa.

Aidha, Day alieleza kuwa Carmudi inaendelea kufanya tafiti mbalimbali zinazohusu unywaji wa pombe uliopitiliza, hali ya magari yaliyopo barabarani na matumizi bora ya barabara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuwezesha kupunguzwa kwa ajali ambazo zingeweza kuepukika kama sheria zilizopo zingefuatwa ipasavyo.

No comments

Powered by Blogger.