GUINEA YAICHAPA UGANDA YA MICHO MABAO 2-0 NA KUFUZU AFCON
Timu ya taifa ya Guinea
imefuzu kucheza Kombe la Mataifa Afrika baada ya kuifunga Uganda mabao 2-0, leo.
Uganda
‘The Cranes’ inayonolewa na Kocha Sredojevic Milutin 'Micho' ikiwa
ugenini, imeshindwa kuonyesha cheche kama mechi iliyopita kwa kukubali
kipigo hicho dhidi ya vijana wa kocha Michel Dussuyer.
Ushindi huo dhidi ya Uganda iliyokuwa na matumaini makubwa, Guinea imefikisha pointi 10 na kufuzu nyuma ya Ghana yenye 11.
Guinea ilipata mabao
yake kila kipindi, la kwanza likifungwa kwa mkwaju wa adhabu ndogo na la pili
mkwaju wa penalti katika kipindi cha pili baada ya beki kisiki na nahodha wa
Uganda, Andy Mwesigwa kufanya madhambi na kulambwa kadi nyekundu.

Post a Comment