ad

ad

AVEVA: TAMBWE HAONDOKI SIMBA



Rais wa Simba, Evance Aveva amesema hawana mpango wa kumwachia mshambuliaji wao, Amissi Tambwe, labda mwenyewe ang’ang’anie kuondoka.

Tambwe, ambaye mkataba wake wa sasa umebakiza miezi sita amekuwa akihusishwa kutakiwa na Yanga tangu alipopoteza namba katika kikosi cha kwanza cha Simba.

Akizungumza na , Aveva alisema uongozi wake upo kwenye harakati za kuongeza nguvu za kikosi chao kwa sasa na si kuwaondoa wachezaji wake nyota. Rais huyo alisema Simba ina idadi kamili ya wachezaji wa kigeni wanaotakiwa kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu zinavyosema na mengine yanayoongelewa ni uzushi tu.

“Tambwe bado mchezaji wetu na wala hatufikirii kumtema labda kama mwenyewe atang’ang’ania kuondoka. Huyo Emeh Izuchukwu mwenyewe ameomba kurejea kwani alishawahi kuichezea klabu hii zamani, lakini  hatuna nafasi ya kumsajili na hao wengine wanaoongelewa ni vyombo vya habari tu vinakuza, lakini hata hatujazungumza nao,” alisema Aveva.

Tambwe alisema kwa sasa yupo mapumzikoni anasubiri muda wa kuanza mazoezi ili arejee Tanzania na kujiunga na wenzake.
Pamoja na kauli hiyo ya Aveva, kumekuwa na taarifa kutoka ndani ya uongozi wa klabu hiyo kwamba baadhi ya viongozi wamekuwa wakitofautiana juu uwepo wa Tambwe, Raphael Kiongera na Pierre Kwizera.

Pia, kulikuwa na taarifa kuwa Kwizera anaweza kutolewa kwa mkopo katika klabu moja nchini Afrika Kusini na nafasi yake kujazwa na mshambuliaji wa Gor Mahia ya Kenya, Dany Sserunkuma.

No comments

Powered by Blogger.