AMFUMANIA MUMEWE, ASAULA!
Stori: Waandishi Wetu
HATARI! Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Tatu Ikoko mkazi wa Mwananyamala jijini Dar, hivi karibuni alifunga mtaa kwa kutembea bila nguo baada ya kumfumania mumewe akiwa na mwanamke mwingine.
Mwanamke anayejulikana kwa jina la Tatu Ikoko akitishia kusaula mbele ya watu.
Chanzo
chetu cha kuaminika kilisema mwanamke huyo aliondoka nyumbani kwake
usiku wa Ijumaa iliyopita na aliporejea asubuhi, alimkuta mwenzake akiwa
na kigori mwingine ndani ndipo alipopagawa.
“Alitoka
usiku mzima akarudi saa moja asubuhi akamkuta bwana’ke yuko na mwanamke
mwingine ndani, akaanzisha vurugu, akavua nguo na kubaki na kanga moja
na kuanza kupita mtaani huku akisema nivue nisivue na watu wakawa
wanamuitikia vua.
Tatu Ikoko akiwa katika hali ya kuvurugwa baada ya kumfuma mumewe na hawara.
“Baada
ya hapo tu watu wazima na mashosti zake walimshika na kumsitiri, akaja
bwana’ke akamchukua wakaenda nyumbani kwao,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo
kiliendelea kufunguka kuwa tukio hilo siyo mara ya kwanza kwa mwanamke
huyo kwani alishawahi kufanya hivyo akiwa na mwanamume mwingine
aliyejulikana kama Kisiso mtaani hapo na waliachana kwa tabia hiyo.
Majirani wakimsitiri Tatu Ikoko.
“Akiwa
na mwanaume halafu akamfumania, ndiyo huwa anafanya hivi na yule
mshikaji wa kwanza kwa aibu ilibidi ahame, sasa hivi anaishi Mbagala,”
kilisema chanzo hicho.imeandikwa na shani ramadhani na mayasa mariwata.


Post a Comment