WEMA, DIAMOND WANADAIWA KUMWAGANA!
Diamond..Mh! Upepo mbaya
unaivumia kapo ya mafahari wawili Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambapo wanadaiwa kufanyiana ‘taimingi’
ya kumwagana.
Staa wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu makini, wawili hao wamepotezeana kwa
muda mrefu huku kila mmoja akifanya yake lakini kila mmoja anashindwa
kujitoa mhanga na kusema hawapo pamoja akihofia kuonekana ndiye tatizo.
“Kifupi ni kwamba Wema na Diamond hawapo pamoja kwa kipindi kirefu,
yawezekana wanawasiliana lakini si kwa mapenzi labda kwa mambo mengine.
Diamond anazuga kama yuko kwenye shoo, hata akirudi Bongo hawana ukaribu
na Wema kama ilivyokuwa zamani, anazuga kidogo kisha anaondoka tena.
Mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platinum.
“Wema naye hivyohivyo, yupo bize na mambo yake, inasemekana yupo na
kigogo f’lani hivi Mkongomani ndiye anampa jeuri mjini kama ulivyoona
juzikati amemwaga mapesa ukumbini.
“Inasemekana Mkongomani huyo
amemfungulia pia ofisi mpya ya kurekodia filamu pamoja na kumnunulia
gari jipya,” kilidai chanzo hicho.
Chanzo hicho kilikwenda mbele zaidi kwa kudai kwamba, Jumapili (jana)
Wema alipanga kutangaza rasmi kumwagana na Diamond wakati alipokuwa
akisherehekea siku yake ya kuzaliwa sambamba na kumtangaza mwanaume wake
mpya.
“Jumapili (jana) ndiyo kila kitu kitakuwa hadharani maana Wema
amepanga kutangaza hadharani kwenye bethidei yake,” kilizidi kudai
chanzo hicho.
Diamond na Wema wakila ujana.
Mwanahabari wetu alipokutana na Wema nyumbani kwake na kumuuliza
kuhusu madai hayo aliyakanusha yote lakini akawa mzito kidogo katika
suala la kutoonana muda mrefu na Diamond.
“Madai yote hayo siyajui!
Nina bwana mpya? Eti kaninunulia gari! Amenifungulia ofisi! Sijui
nimeachana na Diamond! Hayana ukweli wowote,” alisema Wema kwa mshangao
mkubwa.
(CREDIT: GPL)
Endelea kulike: www.facebook.com/2jiachie
Tembelea: www.2jiachie.com
Tembelea: www.2jiachie.com

Post a Comment