WAMBURA AWATAJA WALIOSABABISHA MECHI YA YANGA, SIMBA KUSOGEZWA
Mkurugenzi
wa Mashindano wa TFF, Boniface Wambura amewataka wapenda soka kuvuta
subira hadi kesho ili kujua mechi ya watani iliyoondolewa Oktoba 12
itachezwa lini.
Lakini akasema hakuna chochote kilichosababisha zaidi ya uamuzi wa Benin kutaka kucheza Oktoba 12.
"Tulikuwa tunapambana kupata mechi, Benin waliona siku hiyo ndiyo wana nafasi.
"Ukizingatia imo ndani ya kalenda ya Fifa, sasa nafikiri hakuna kosa lolote," alisema Wambura.
"Watu
wavute subira, tutawatangazia Leo lini mechi hiyo itachezwa. Usiku wa kuamkia leo walikutana na bodi ya ligi kulijadili suala hilo."
Mashabiki
wamekuwa wakilalamika kwamba kusogezwa kwa mechi hiyo kunaashiria
kubebwa kwa Simba iliyokuwa ina wachezaji wengi majeruhi.

Post a Comment