ad

ad

MARIA - 04

 Endelea kulike ==>www.facebook.com/2jiachie
MTUNZI: Nyemo
“Samahanini..” Maria aliwaambia wanawake ambao walikuwa wakichota maji katika kisima kimojawapo kijijini hapo.
   Wakinamama wote wakaacha kuchota maji, wakaanza kumwangalia Maria ambaye kwa muonekano tu alionekana kuchoka.
   “Naomba mnisaidie chakula. Nimetoka mbali, nimeshinda pasipo kula usiku kucha mpaka sasa hivi Maria aliwaambia wakinamama wale.
   Tayari machozi yalikwishaanza kumlenga na baada ya muda yakaanza kutiririka mashavuni mwake. Maria alionekana kuchoka na kuhitaji msaada wa chakula kwa wakti huo. Mwanamke mmoja akaanza kumsogelea Maria na kuanza kumwangalia usoni kana kwamba alikuwa akimfananisha na mtu fulani.

   “Usihofu binti. Pole sana kwa matatizo, twende nyumbani ukale” Mwanamke yule alimwambia Maria na kisha wote wawili kuanza kuondoka mahali hapo.
   Mwendo wala haukuwa mrefu, wakafika katika nyumba ya udongo na kuingia ndani. Ndani ya nyumba hiyo hakukuwa kukivutia hata kidogo, kila kitu kilionekana kuwa shaghalabaghala. Maria akakisogelea kitanda cha kamba na kutulia.
   Mwanamke yule akaelekea katika chumba kingine na baada ya muda akarudi mahali hapo akiwa na sufuria iliyokuwa na chakula cha jana pamoja na birika ya chai na kisha kumgawia Maria. Ingawa chakula kilikuwa cha baridi lakini Maria hakuonekana kujali kitu chochote kile, akaanza kukila kwa haraka haraka.
   “Hivi hapa si ndio Mkuyuni Maria alimuuliza mwanamke yule.
   “Hapana binti yangu, hiki ni kijiji cha Semakwede” Mwanamke yule alimwambia.
   Maria akaanza kuelezea kila kitu ambacho kilitkea katika maisha yake, kuanzia alipokuwa akisoma mpaka alipopewa ujauzito. Mwanamke yule aliyejitambulisha kwa jina la Bi Semeni alibaki kimya huku akimsikiliza kwa makini.
   Maria alielezea kila kitu, hakutaka kuficha kitu chochote kile. Bi Semeni akaonekana kuhuzunika, historia ya Maria ilionekana kumgusa kupita kiasi. Kitu alichokifanya ni kuanza maisha pamoja na Maria, akamkaribisha nyumbani hapo kukaa nae.
                                                                           ********
   Jina la Bi Semeni halikuwa geni katika masikio ya wanakijiji waliokuwa wakiishi katika kijiji cha Semakwede. Bi Semeni alikuwa maarufu kijijini hapo kutokana na biashara ya pombe haramu ya gongo ambayo alikuwa akiifanya kijijini hapo. Wanakijiji wengi walikuwa wateja zake, kila kitu kilikuwa kikipatikana kilabuni hapo, kilabu yake ndio ambayo ilikuwa maarufu sana kwa kila mtu kijini hapo na hata vijiji vya jirani.
   Hakukuwa na polisi yeyote ambaye alikuwa akifuatilia bishara hiyo ambayo ilikuwa ikimuingizia fedha nyingi, kila polisi ambaye alionekana kufuatilia, ni rushwa tu ndio ambayo ilikuwa ikitumika. Ingawa biashara yake ilikuwa haramu lakini ndio ambayo ilikuwa ikiendesha maisha yake ya kila siku.
   Alikuwa akinunua mavazi, chakula na hata kuwalisha ndugu zake wengine pamoja na wajukuu zake kupitia biashara hiyo ambayo ilikuwa ikijipatia idadi kubwa ya wateja kila siku. Bi Semeni alionekana kutokuwa na mpinzani katika biashara hiyo, kila siku jina lake lilikuwa juu.
   Mwezi mmoja ulikuwa umepita tangu Maria afike katika nyumba ya Bi Semeni ambayo ilikuwa katika kijiji hicho cha Semakwede. Yeye ndiye ambaye alikuwa akimsaidia Bi Semeni katika kila kazi ambayo aliiona inafaa kusaidiwa. Japokuwa Maria alikuwa amelelewa katika familia iliyomjua Mungu, lakini akajikuta nae akianza kazi ya kutengeneza pombe hiyo haramu.
   Kila siku maisha yake aliyaona yakianza kubadilika, pamoja na kumsaidia Bi Semeni kutengeneza pombe lakini nae akaanza kuonja. Kila siku alikuwa muonjaji mpaka kufikia kipindi ambacho nae akawa mnywaji.
   Maria alionekana kusahau kabisa kule alipotoka, maisha mapya yakaonekaa kuchukua nafasi kubwa katika maisha yake. Ujauzito wake haukuwa na matatizo yoyote yale, kila siku alipata chakula kizuri kwa afya ya mtoto wake.
   Bi Semeni akatokea kumpenda Maria kuliko mtu yeyote ambaye alikuwa akiishi nae nyumbani kwake, hiyo ilitokana na jinsi ambavyo Maria alivyokuwa akijituma katika kufanya kazi nyumbani hapo.
   Matatizo ya walevi bado yalikuwa yakiendelea kila siku, kushikwa makalio mara kwa mara ilionekana kuwa moja ya maisha yake ambayo baadae alikuja kuyazoea. Kila siku alikuwa akitukanwa na walevi pasipo kujua sababu ambayo iliwapelekea kumtukana, Maria hakujibu chochote kile, kila siku alikuwa mvumilivu.
   Bado uzuri wa Maria ambao alikuwa nao katika kipindi cha nyuma alikuwa nao mpaka muda huo. Kila siku vijana wa kijijini hapo walikuwa wakimuwinda Maria. Maria hakuonekana kuwa rahisi kuwakubalia wavulana, kila siku alikuwa akiwakataa.
   Wavulana zaidi ya ishirini ambao walikuwa wakimtaka Maria walikuwa wamekataliwa jambo ambalo baadhi yao waliona ilikuwa bora kufanya kitu ambacho kilikuwa ni kama kumkomoa.
   “Mnaonaje kama tukimbaka?” Kijana mmoja aliwaambia wenzake.
   “Hilo ni wazo zuri, lakini kama akitujua na kwenda kutushitaki! Hamuoni kuwa hilo litakuwa tatizo kwetu?” Kijana mwingine aliuliza.
   “Sheria za kijiji hiki ziko mikononi mwetu Mtula, acha woga wako, kama unaogopa basi usishiriki” Kijana mwingine alimwambia Mtula.
   “Kuogopa siogopi, kama ndio hivyo basi sawa” Mtula aliwaambia.
   Hayo ndio makubaliano ambayo yalipangwa na vijana wanne ambao walikuwa miongoni mwa vijana waliokuwa wamemfuatilia Maria kwa kipindi kirefu pasipo mafanikio yoyote. Wote walipanga kitu kimoja ambacho kilipewa nafasi kubwa ndani ya mioyo yao, kumbaka Maria.
   Usiku wa siku hiyo vijana wale walikuwa wamejikusanya nyuma ya nyumba ya Bi Semeni, macho yao hayakuweza kutulia sehemu moja, kila wakati walikuwa wakiangalia katika kila pande katika maeneo ya nyumba ile.
   Kelele za walevi ambao walikuwa wakiendelea kunywa pombe katika kilabu cha Bi Semeni bado zilikuwa zikiendelea kusikika masikioni mwao hali iliyowafanya kugundua kuwa bado Maria alikuwa ndani ya kilabu kile akiendelea kutoa huduma.
   Waliendelea kusubiri zaidi na zaidi, kila mmoja alikuwa na imani kuwa ni lazima Maria angetoka nje hali ambayo ingewafanya kumfuata na kumfanyia kile ambacho walikuwa wamedhamiria kufanya katika usiku ule.
   Kila mtu alikuwa na hamu ya kukutana kimwili na Maria, umbo lake pamoja na uzuri wake vilikuwa ni vitu ambavyo vilikuwa vikiendelea kuwavutia kupita kawaida. Dakika ziliendelea kwenda mbele lakini Maria hakuonekana mahali hapo kitu ambacho kilimfanya kila mtu kukata tamaa.
   “Kama vipi tufanyeni hata kesho kuliko kuendelea kubaki hapa kichakani?” Mtula aliwaambia.
   “Hata kama atachelewa kutoka, hapa hatuondoki” Kijana mmoja alimwamba Mtula.
   Muda ulizidi kwenda mbele laki Maria hakuwa ameonekana machoni mwao. Walitaka kuliahirisha zoezi lao lakini hata kabla hawajaamua moja kwa moja wakaanza kujawa na furaha mara baada ya kumuona Maria akitoka nje ya kilabu kile huku akiwa ameshika kopo kubwa ambalo walevi walikuwa wakilitumia kunywea pombe ile haramu.
   Kwa mwendo wa hraka haraka na wa kunyata vijana wale wakaanza kumsogelea Maria kule alipokuwa amesimama, walipomfikia, wakamvamia, vijana wawili wakamshika miguu na mikono huku wengine wakimfumba mdomo na kuanza kuondoka nae kuelekea kichakani.
   Maria alikuwa akikurupuka kama njia mojawapo ya kutaka kujinasua kutoka katika mikono ya vijana wale, vijana wale walionekana kumshika vilivyo. Maria alijitahidi kutoa sauti za kuomba msaada lakini hakukuwa na sauti yoyote iliyokuwa ikisikika zaidi ya muungurumo tu.
   Vijana wale walimpeleka Maria mbali kidogo na eneo la nyumba za pae kijijini, wakamlaza juu ya nyasi na kumwangalia huku kila mmoja akijiandaa kuvua suruali.
   “Nisaidieeniii... Nisaidieniiii...” Maria alipiga kelele za kuomba msaada lakini hakukuwa na mwanakijiji yeyote ambaye alizisikia kelele zile kutokana na umbali wa mahali pale kutoka kijijini.
   Maria akabaki akiomba msamaha japokuwa hakuwa akilifahamu kosa ambalo alilifanya. Hakukuwa na mtu yeyote ambaye alionekana kujali chochote kile, kila mmoja katika kipindi hicho alikuwa na uchu wa kufanya ngono tu.
   “Nani anaanza?” Kijana mmoja aliuliza.
   “Mimi” Mtula alijibu haraka haraka kama mtu aliyetaka kuwahi mahali fulani.
   “Ukitoka wewe zamu yangu” Kijana mwingine alimwambia Mtula.
   Kasi aliyoitumia Mtula kuivua suruali yake ilikuwa kubwa ambayo hata vijana wenzake walibaki wakishangaa. Mtula akabaki mtupu kama alivyozalia, vijana wengine wakamvua Maria sketi ambayo alikuwa ameivaa.
   “Bado nini?”
   “Nguo ya ndani”
   Maria akavuliwa nguo ya ndani kilazima na kubaki mtupu. Alijitahidi kuendelea kupiga kelele za kuomba msaada lakini hakukuwa na mtu yeyote aliyezisikia kelele zile. Maria akabaki akilia tu, alijiona kutokuwa na ujanja wa kutoka katika mikono ya vijana wale.
   Ingawa kichakani pale kulikuwa na giza totoro lakini Mtula alikuwa akiuona mwili wa Maria vizuri kabisa kana kwamba alikuwa akimmulika kwa tochi. Pasipo kupoteza muda wowote ule, Mtula akamlalia Maria na kuanza kumbaka huku vijana wengine wakiwa wamemshika mikono.
   Wagonjwa wale waliendelea kubaki hospitalini kwa muda wa mwezi mmoja. Mmoja alionekana kuwa na nafuu huku yule mwingine akionekana kuwa mahututi. Hali yake ilionekana kumkatisha tamaa kila daktari ambaye alikuwa akimwangalia.
   Mgonjwa yule alionekana kuanza kuishi katika maisha ya matumaini, tayari alianza kuonekana mfu aliyekuwa akipumua. Madaktari walipoona hali yake inazidi kuwa mbaya, ikawabidi wamuamishie mgonjwa yule aliyapata nafuu katika chumba kingine.
   Wiki zaidi ikapita na hatimae mgonjwa yule aliyekuwa nafuu kidogo akaanza kufumbua macho. Kila kitu ambacho alikuwa akikiona mahali hapo alikuwa akishangaa, hakuelewa ni kwa jinsi gani alikuwa amefika mahali hapo.
   Dripu mbili za maji zilikuwa zimetundikwa pembeni mwa kitanda chake, maji yalikuwa yakiingia mwilini mwake taratibu kupitia katika mishipa yake. Akabak kwa muda huku akionekana kufikiria vitu fulani. Picha ya tukio ambalo lilimfanya kufika mahali hapo ikaanza kumjia.
   “Amefumbua macho” Sauti ya nesi ilisikika.
   Kwa kasi ya ajabu nesi yule akaanza kukimbia kuelekea nje. Breki yake ya kwanza ilikuwa katika ofisi ya dokta mkuu, Dokta Manase. Hakugonga hodi mlangoni, akaingia moja kwa moja.
   “Mgonjwa amefumbua macho” Nesi alimwambia dokta Manase.
   “Mgonjwa gani?”
   “Yule aliyepata ajali” Nesi alijibu.
   Dokta hakutaka kuendelea kubaki ofisini mwake, kwa haraka haraka akasimama na kuanza kuelekea katika chumba alichokuwa mgonjwa yule. Dokta akaonyesha tabasamu pana, akaonekana kufurahishwa na hali aliyokuwa nayo mgonjwa yule.
   “Safi sana. Tundikeni dripu nyingine” Dokta waliwaambia manesi ambao walikuwa ndani ya chumba kile. Dripu mbili zaidi zikatundikwa.
   “Mwacheni apumzike kwanza, msimwambie chochote kile juu ya rafiki yake” Dokta Manase aliwaambia manesi.
   Mgonjwa yule aliendelea kubaki hospitalini huku akizidi kujisikia nafuu kadri siku zilivyozidi kwenda mbele. Kila siku mawazo juu ya ajali iliyotokea ilikuwa ikimwandama, alijua fika kwamba walikwa wawili ndani ya gari kabla ya gari kupata ajali, mwenzake alikuwa wapi?
   Kila alipokuwa akiuliza kuhusu rafiki yake, manesi hawakujibu kitu, walibaki kimya kana kwamba hawakuwa wamesikia swali lile. Hali ile ikamfanya mgonjwa yule kukosa amani, kila siku alikuwa mtu wa mawazo tu.
   “Mbona hautaki kunijibu?” Mgonjwa yule alimuuliza nesi.
   “Subiri kwanza, jina lako nani?” Nesi yule alimuuliza.
   “Naitwa Onesmo Samsoni” Mgonjwa yule alijibu na nesi kuandika.
   Nesi akaanza kupiga hatua kuufuata mlango. Hakuonekana kuwa tayari kuongea kitu chchote kuhusu mgonjwa yule ambaye katika kipindi cha nyuma alikuwa mahututi, alibaki kimya huku akimtaka dokta Manase mwenyewe amwambie mgonjwa yule.
   “Nesiiiii...”Onesmo aliita na nesi kugeuka.
   “Niambie ukweli, mbona kila siku mnanificha?”
   “Ukweli gani?”
   “Juu ya rafiki yangu. Najua anaweza akawa amefariki, najua kwamba ilikuwa ni ajali mbaya ambayo iligonga zaidi katika upande aliokuwa amekaa yeye. Niambie ukweli nesi. Hata kama amefariki, wewe niambie tu. Kumbuka kuwa mimi ni mwanaume” Onesmo alimwambia nesi.
   Nesi hakusema kitu chochote, alibaki akimwangalia Onesmo huku macho yake yakionekana yakilengwa na machozi. Nesi alitamani kuongea kitu lakini kila alipokuwa akimfikiria dokta Manase, alibaki kimya.
   “Nesiiiiii.... nesiiiiii....” Onesmo aliita katika kipindi ambacho nesi alimua kuondoka chubani mule.
   Kila dalili za Issa kufariki dunia zilikuwa zimekwishajinyesha. Kila siku Onesmo alibaki mpweke, ajali ile ilionekana kumhuzunisha kupita kiasi.
   Siku ziliendelea kwenda mbele mpaka pale dokta Manase alipoamua kumwambia ukweli juu ya rafiki yake, Issa. Onesmo hakuonekana kusikitika sana kutkana na kulifahamu hilo kitambo. Alibaki na majonzi ya kawaida ambayo wala hayakumtoa machozi.
   “Kwa nini mlikuwa mkinificha?”
   “Tulitaka upate nafuu, Onesmo. Kama tungekwambia ukweli, basi ni lazima ungelia na kuzifanya nyuzi tulizokushona kufumuka” Dokta Manase alimwabia Onesmo.
   Dokta Manase akabaki akimfariji Onesmo kwa kumkumbatia huku akimpiga piga mgongoni. Japokuwa Onesmo hakuwa akihuzunika sana lakini dokta aliamua kufanya hivyo ili kumuonyeshea ni kwa jinsi gani alikuwa akimjali.
   “Utaendelea kubaki mahali hapa kwa wiki moja zaidi. Usihofu, hali yako itaudi na kuwa kama kawaida” Dokta alimwambia Onesmo.
                                            
   Maria alisikia maumivu makali sehemu za siri. Vijana wanne ambao walikuwa wamemuingilia walikuwa wamemsababishia maumivu hayo mpaka kuzifanya damu kuanza kumtoka. Maria alibaki akilia pale kichakani, alishindwa kuinuka kabisa.
   Akaanza kutambaa kana kwamba alikuwa amepigwa risasi miguuni. Hali ilionekana kuwa mbaya kupita kawaida. Kadri muda ulivyozidi kwenda mbele na ndivyo ambavyo damu zilivyozidi kumtoka.
   Maria alizidi kujisikia maumivu tumboni mwake, aliendelea kutambaa zaidi na zaidi huku maumivu yale yakizidi kuongezeka zaidi. Maria akashindwa kuendelea zaidi, macho yake yakazidi kujaa giza, hapo hapo akapoteza fahamu pasipo kufahamu ni kitu gani ambacho kilikuwa kimeendelea.
   Maria alikuja kupata fahamu baada ya masaa nane kupita. Alijikuta yuko kitandani ndani ya chumba ambacho alikuwa akikitumia nyumbani kwa Bi Semeni. Kitu cha kwanza ambacho alikuwa amekihisi mwilini mwake ni maumivu ambayo yalikuwa yameanza kupungua.
   Maria akainuka na kukaa kitako kitandani. Sauti za ndege zaikaanza kusikika huku mwanga ukianza kuonekana nje hali ambayo ilimuonyeshea kuwa asubuhi ilikuwa imeingia. Maria akakaa kitako, akaanza kulia tena.

Endelea kulike ==>www.facebook.com/2jiachie
ITAENDELEA SIKU YA KESHO

No comments

Powered by Blogger.