MADEE MBARONI AKIHUSISHWA NA UTEKAJI
Rais wa Manzese ambaye ni staa wa Bongo Fleva, Hamad Ally ‘Madee’
amelala nyumba ya nondo za mahabusu baada ya kutiwa mbaroni akihusishwa
na utekaji wa dereva wa bodaboda, Suedi Waziri (pichani) kisha kumpa
kipigo cha mbwa mwizi.
Rais wa Manzese ambaye ni staa wa Bongo Fleva, Hamad Ally ‘Madee’.
Akizungumza na gazeti hili, mmiliki wa bodaboda iliyokuwa ikiendeshwa
na Waziri ambaye ni msanii wa filamu na Mkurugenzi wa Hamadombe
Distributor, Fatuma Makame ‘Joanita’ alisema tukio hilo lilitokea
Jumapili iliyopita ambapo Madee alikuwa akifanya shoo katika Ukumbi wa
Kumbia Pub uliopo Vijibweni Kigamboni, Dar.
Kwa mujibu wa shushushu wetu, baada ya Madee kumaliza shoo ukumbini
hapo, mashabiki walimsindikiza kwa shangwe ambapo gari lake lilikuwa
katika mwendo wa taratibu ndipo Waziri aliyekuwa amempakia abiria nyuma,
abiria huyo wake akadaiwa kukwapua simu ya msanii huyo na kutokomea
kusikojulikana.
Dereva wa bodaboda, Suedi Waziri anayedaiwa kutekwa na staa wa Bongo Fleva, Hamad Ally ‘Madee’.
Ilidaiwa kwamba Waziri alibaki akiwa amepigwa butwaa baada ya tukio
hilo kwani wakati anampakia abiria huyo hakujua ni kibaka ambapo akiwa
ameduwaa, alishangaa kupokea kipigo kikali kutoka kwa Madee na wenzake
ambapo walimchukua na pikipiki yake wakampeleka hadi nyumbani kwa Madee,
Manzese, Dar kisha kumpa mateso kuanzia saa 2:00 usiku hadi saa 8:00
usiku.
Iliendelea kudaiwa kwamba asubuhi iliyofuata akina Madee walimpigia
simu mama mdogo wa Waziri na kumtaka apeleke fedha kwa ajili ya
kununulia simu kwani mwanaye alikuwa amekwapua simu ambapo mama huyo
alifika katika Kituo cha Polisi cha Magomeni, Dar na kutoa taarifa.
Ilisemekana kwamba mama huyo aliwachukua polisi wa difenda kisha
akatimba nao Manzese kwa Madee na kumchukua kijana huyo akiwa na maumivu
makali kwani alikuwa amechanwa na viwembe lakini wahusika walikimbia.
Joanita aliendelea kusema baada ya hapo, Madee alikwenda kuripoti
polisi Magomeni ambao walimwambia anatakiwa akatoe taarifa hizo kwenye
Kituo cha Polisi cha Kigamboni kwani ndipo tukio lilipotokea.
Alisema kwamba Madee alifanya hivyo bila ubishi na hapo ndipo
aliposwekwa lupango na kulala huko japokuwa jamaa zake walifanya
jitihada za kumtoa lakini ikashindikana.
Madee amefunguliwa shitaka katika Kituo cha Polisi cha Kigamboni kwa jalada namba VJB/RB/625/2014
Madee amefunguliwa shitaka katika Kituo cha Polisi cha Kigamboni kwa jalada namba VJB/RB/625/2014
KUTEKWA KWA BINADAMU.
Wakati gazeti hili linakwenda mitamboni polisi walikuwa wakikagua nyumbani kwa Madee na kuona sehemu ambayo kijana huyo alikuwa akiteswa huku simu ya Madee ikiita bila kupokelewa.
Habari zinadai msanii Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ naye anasakwa na polisi kuhusiana na tukio hilo kwa sababu alikuwa na Madee.
Wakati gazeti hili linakwenda mitamboni polisi walikuwa wakikagua nyumbani kwa Madee na kuona sehemu ambayo kijana huyo alikuwa akiteswa huku simu ya Madee ikiita bila kupokelewa.
Habari zinadai msanii Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ naye anasakwa na polisi kuhusiana na tukio hilo kwa sababu alikuwa na Madee.
CHANZO: GPL

Post a Comment