LIVERPOOL YABANWA 2-2 NA BORO KOMBE LA LIGI, YATOKEA KWENYE PENALTI 14-13 ANFIELD
KLABU
ya Liverpool imeifunga Middlesbrough kwa penalti 14-13 katika Raundi ya
Tatu ya Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One Cup kufuatia sare ya
2-2 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Anfield.
Kinda
Jordan Rossiter alianza kuwafungia Wekundu hao baada ya kupewa nafasi
ya kwanza kuchezea kikosi cha kwanza, kabla ya Adam Reach kuwasawazishia
wageni akimalizia pasi ya Grant Leadbitter.
Mchezo huo ulihamia kwenye muda wa nyongeza kufuatia timu kumaliza zikiwa zimefungana 1-1 baada ya dakika 90.
Suso
akafunga bao lake la kwanza tangu ajiunge na Liverpool kuwapatia bao la
kuongoza Wekundu hao, lakini Kolo Toure akacheza rafu ndani ya boksi
na Patrick Bamford akaenda kusawazisha dakika za lala salama na katika
penalty Liverpool ikashinda 14-13 baada ya Albert Adomah kupoteza mkwaju
wa Boro.
Kikosi
cha Liverpool kilikuwa; Mignolet, Manquillo, Toure, Sakho, Enrique,
Rossiter/Williams dk79, Lucas, Sterling, Lallana, Markovic na
Lambert/Balotelli dk74.
Middlesbrough; Blackman, Fredericks, Ayala, Omeru, Friend, Adomah, Clayton, Leadbitter, Reach, Tomlin na Kike/Wildschut dk76.
![]() |
| Mario Balotelli akipambana jana Anfield |
![]() |
| Wachezaji wa Liverpool wakishangilia ushindi wao jana |



Post a Comment