DOWNLOAD MAN WATER & MBATIZAJI - WIFE MATERIAL
The Producers,ni kundi la Muziki,linaloundwa na wanamuziki wawili,ambao ni MBATIZAJI pamoja
na MAN WATER.Kundi hili limeanza kusambaza wimbo wake mpya unaojulikna
kwa jina la "WIFE MATERIAL" katika vituo mbalimbali vya radio vilivyopo
nnchini Tanzania na nje ya nchi.
Wimbo wa WIFE MATERIAL umerekodiwa katika Studio mbili,FLEXIBLE MUSIC
ambayo Producer wa studio hiyo ni MBATIZAJI,pamoja na COMBINATION SOUND
ambapo producer wa studio hiyo ni MAN WATER.
Watayarishaji wa muziki hawa,waliamua kuanza kufanya kazi pamoja kipindi cha miaka ya
2004,walipokutana mkoani Morogoro.Na ilipofikia miaka ya 2011 waliweza
kufanya nyimbo iliyojulikana kwa jina la "HESHIMA KAZI",nyimbo
iliyofanya vizuri katika vituo mbalimbali vya radio pamoja na TV.
Baada ya kimya kirefu sasa THE PRODUCERz,wamerudi tena na nyimbo
nyengine,ambapo kwa sasa wanasambaza Audio ya nyimbo hiyo,huku wakiwa
katika maandalizi ya kufanya video ya wimbo huo hivi
WIFE MATERIAL ni nyimbo yenye ujumbe mzuri ambao unaweza kusikilizwa na
rika lolote,na ni wimbo unaoburudisha na kufundisha pia.Kwa sasa wimbo
huo unapatikana katika mitandao mbalilmbali ya kijamii,na unasikika
katika vituo mbalimbali vya radio.
Sikiliza WIFE MATERIAL hapa chini kupata radha toka kwa THE PRODUCERz.....
karibuni.

Post a Comment