ad

ad

VITILIVYOGO (PAPA NA MUHOGO) - 12

“Hebu tulia, twende.”
Edna alimshika mkono na kutoka naye nje, alipofika sebuleni alipitia noti ya elfu tano iliyokuwa juu ya meza.
“Nitakupa hela ukaninunulie dawa.”
“Kisha nilete?” Shaka alishtuka.
“Hapana, usinunue wala nini wewe nenda zako natumia njia ya kukutoa ili mume wangu asijue chochote.”
“Sawa.”
Alifungua mlango na kusema kwa sauti iliyowafanya wote waangalie akiwemo mumewe.
“Shaka kaninunulie dawa ya kichwa fanya haraka,” alimpa noti ya elfu tano.
Alimpa hela ile mbele ya macho ya watu, kauli ile ilimshtua mumewe na kuuliza.
“Vipi honey unaumwa?”
“Shaka hebu wahi dukani,”  Edna alimtoa kwanza Shaka ndipo azungumze na mumewe.
Shaka aliondoka  kwa kukimbia kwa vile alikuwa hajiamini alijikwaa na kuanguka.
“Shaka taratibu jamani siyo haraka kihivyoo.”
Shaka alinyanyuka bila kusema na kutokomea zake, baada ya kuondoka eneo lile aliona kama ametoka katika mdomo wa simba na kuapa hatafanya tena mapenzi na Edna.
Shaka hakujiamini mpaka alipofika nyumbani kwao, hakukaa, aliondoka kuogopa kutafutwa na mume wa Edna. Alirudi nyumbani majira ya saa nne usiku na kuingia ndani kimyakimya bila kula na kujifungia ndani.
Betty alirudi usiku mkubwa na kumgongea Shaka aliyekuwa amelala. Kwanza moyo ulimlipuka na kujua amefuatwa na mume wa Edna. Lakini sauti ya Betty ilimshusha pumzi zake.
Alipojaribu kujigeuza mwili ulikuwa umechoka sana kutokana na kazi ya kuulaza chini mbuyu kwa panga. Pamoja na kuchoshwa sana na Edna hakutaka kutoka usiku ule kwenda kwa Betty kwa kujua lazima atachemsha kwani wote walikuwa na miili mikubwa na nguvu kama nyati tofauti na Stella na Diana. Ili asiondoke na Betty alisingizia ugonjwa.
“Bebi naharisha.”
“Shaaaka! Mpenzi wangu jitahidi hata kidogo.”
“Betty yaani hata nguvu sina.”
“Shaka si heri ningekwenda kulala na Jimmy!”
“Bebi vumilia kwa leo.”
“Yaani Shaka hali ni mbaya mipombe niliyokunywa yote imekimbilia chini,” Betty alisema kwa sauti ya kilevi.
“Bebi naomba unielewe, usinigeuze chombo chako cha starehe,” Shaka alijifanya kuwa mkali.
“Jamani Shaka yamekuwa hayo!”
“Ni wazi Betty hunipendi bali unataka kunigeuza chombo cha kumaliza hamu zako.”
“Siyo hivyo Shaka, mpenzi wangu nilijua unakuja kumaliza hamu zangu na kumkacha Jimmy kwa kusingizia ugonjwa ili nije kwako mpenzi wangu.”
“Ndiyo hivyo hali yangu leo tata, nina imani unanijua vizuri.”
“Mmh! Sawa nitafanyaje?” Betty alikubali kwa shingo upande.
Shaka ili kuonesha anaharisha alikimbilia msalani, alitulia kwa muda na kurudi huku ameinama ameshikilia tumbo.
“Vipi Shaka tumbo linauma sana?”
“Yaani wee acha tu.”
“Basi nikupeleke hospitali.”
“Acha tu nimeshameza dawa acha nilale tuangalie kesho.”
“Pole sana mpenzi wangu,” Betty alisema kwa sauti ya huruma.
“Asante.”
“Basi  mpenzi kalale tutaonana kesho.”
“Usiku mwema.”
Betty aliondoka roho ikiwa haimpi kabisa kutokana na kupandwa na maruhani nyumbani alipaona pachungu alikodi gari kwenda kulala kwa mpenzi wake.
                               ***
Siku ya pili Shaka alikwenda shule, kama kawaida Stella aliendelea kuwa naye karibu. Wakati wa mapumziko Stella akiwa amekaa na Shaka na shoga yake Diana. Alimwambia maneno ambayo yalikuwa mkuki moyoni kwa shoga yake.
“Bebi hamu zangu za jana leo nataka ukazimalize.”
“Hakuna tatizo.”
“Yaani jana nililala vibaya baada ya kuondoka ghafla wakati nikijua ilikuwa zamu yangu.”
“Kwani una zamu na nani?” Shaka alishtuka.
“Si kwa vile siku nyingine unawahi nyumbani.”
“Basi mama leo kazi ni kwako kama Voda.”
“Waaawooo mpenzi wangu,” Stella alimkumbatia  Shaka bila kuogopa wanafunzi wenzao waliokuwepo wakipata vinywaji.
  Jioni ya siku ile Stella alimlazimisha shoga yake amsindikize.  Wakati wanajiandaa kuondoka Shaka aliitwa ofisini na mwalimu na kuwafanya  watangulie nje kumsubiri.
Muda ulikwenda bila shaka kuonekana, Diana alimshauri Stella waondoke.
“Stella tutakaa mpaka saa ngapi huoni kama Shaka anaweza kuchelewa.”
“Tatizo lipo wapi, kama nakuchelewesha unaweza kuwahi,” Stella alijibu kwa hasira.
“Sina maana hiyo, kwani shida yako kuzungumza tu au kurusha roho kabisa?”
“Shoga nina ugwadu kama nimetoka gerezani.”
“Mmh! Si mtakesha?”
“Walaa, leo atanipa penzi jepesi ili niwahi nyumbani.”
“Mmh! Ninavyomjua Shaka akionja utataka tena.”
“Hamna kidogo tu.”
“Usinidanganye Shaka si mwanaume wa kuonja kidogo ukaridhika.”
“Umejuaje, shoga tunazungukana nini?”
“Aah..noo kwani vipi?” Diana alijikuta akipata kigugumizi baada ya kujisahau na kuchanganya madawa.
“Hapana umejuaje uwezo wa Shaka kama siyo kuzungukana?”
“Jamani Diana si ni wewe uliyenieleza kuwa Shaka ukikutana naye huwa hutamani muachane upesi.”
“Ooh! Kweli nilikuwa na wasiwasi unatia mkono kwenye mzinga wangu ya nyuki kulamba asali yangu.”
“Jamani shoga wanaume wote wameisha mpaka nimchukue mpenzi wako, kwanza Shaka kwangu mtoto mdogo.”
“Mdogo kwako lakini kwangu mkubwa mwenzangu.”
“Mmh! Tena huyoo anakuja,” Diana alisema baada ya kumuona Shaka kwa mbali akija.
“Diana tuachane na habari za Shaka asije kusema tukiwa peke yetu kazi yetu kumsema,” Stella alimwambia Diana.
“Mmh! Sawa.”
Wakati huo Shaka alikuwa amefika na kwenda moja kwa moja kwa Stella na kumbusu shavuni.
“Samahani sweet kuna somo nilikuwa naelekezwa na mwalimu ambalo sikulifanya vizuri.”
“Mmh! Sawa, ndiyo mwaka mzima?” Stella alilia wivu.
“Jamani kwanza tuliofanya vibaya tulipewa adhabu ya  kuokota uchafu kisha nikaitwa ofisini kwa maelekezo.”
“Ofisini kulikuwa na walimu wangapi?”
“Watatu,” Shaka aliongopa ili kumfanya Stella asiwaze vingine.
“Sasa?”
“Nakusikiliza mama,” Shaka alijibu huku amtupia jicho Diana aliyebinua midomo kwa wivu.
“Nataka akanipe nusu dozi.”
“Wewe tu mimi tivii rimoti yangu ni wewe.”
“Diana twende zetu basi,” Stella alisema huku akinyanyuka kwenye kiti.
“Wapi?” Shaka aliuliza.
“Pa siku zote.”
“Sasa Stella mi si niende nyumbani tu,” Diana alimwambia shoga yake kwa kuamini ugwadu wake na utundu wa Shaka lazima wangekesha.
“Diana mbona leo sikuelewi tumekubaliana vipi, si nimekueleza hata nikichelewa nitarudi na wewe nyumbani ili nipate kujitetea.”
“Mi namjua Shaka akikushika huwezi kunikumbuka na kunifanya nikae niking’aa macho.”
“Mbona sikuelewi maneno yako yanaonesha kuna vitu vya Shaka unavielewa tofauti na nilivyokueleza.”
“Kwa sababu gani?”
“Kwa nini ung’ang’anie akinishika siwezi kutoka upesi?”
“Jamani, hivi unavyosema una ugwadu ni penzi jepesi tu mnaachana, lazima pachimbike bila jembe,” Diana alitengeneza uongo uliokubalika.
“Mimi si ndiye niliyekueleza nitawahi kutoka, vilevile Shaka anatakiwa kuwahi nyumbani kwao.”
“Kwani tatizo nini, kama ana haraka anaweza kwenda,” Shaka alisema.
“Shaka, Diana ni mtu muhimu sana nikichelewa kurudi nyumbani nikienda naye napata sababu ya kujitetea.”
“Sasa kama anajua hivyo mbona analeta mashauzi?” Shaka alijifanya kukasirika Diana.
“Basi shemu nitawasubiri,” Diana alikubali shingo upande.
Walikodi teksi hadi kwenye uwanja wa nyumbani, Shaka na Stella waliingia ndani  na kumwacha sehemu Diana akisubiri huku donge la wivu likiwa limemtanda kwa kujua shoga yake anakwenda kufaidi mautundu ya Shaka.
Baada ya kuingia ndani, Stella alionekana ana uchu wa fisi, baada ya kuingia tu alimvamia Shaka na kumsaula kisha naye alisaula na kwenda naye bafuni kuoga. Shaka akiwa na matirio mapya alianzia kumpa mshikemshike kulekule bafuni kama alivyofundishwa na Betty.
Stella alizidi kuchanganyikiwa baada ya kulizwa machozi mawili bila msiba.
“Jamaniii.. Shaka yote haya umeyajulia wapi?”
“Kwa nini?”
“Si Shaka yule niliyekuwa nikijitahidi kumfundisha, sasa hivi wewe ni mwalimu tena mwalimu wa walimu.”
“Mmh! Kwa nini?”
“Huku hivi, kitandani sijui itakuwaje? Shaka kubali unioe.”
“Nitakuoa tukimaliza masomo.”
“Hapana Shaka tufunge hata ndoa ya siri.”
“Tutapanga.”
Baada ya kutoka bafuni Shaka akiwa mpya tofauti na aliyemzoea alimchanganya. Kila alichokifanya kulibadili raha na utamu. Baada ya kuchanganywa na utundu wa Shaka, Stella alijikuta akiangua kilio.”
“Unalia nini tena baby?” Shaka aliuliza.
“Kwa nini unampa raha zangu Diana?”
“Diana?” Shaka alishtuka.
“Ina maana hujui, nani kamwambia kuwa wewe mtamu?”
“Stella si shoga yako kakuumbua mbele yangu, kumbe tunachofanya unakwenda kumwambia shoga yako.”
“Muongo... muongo mkubwa yule,” Stella alijitetea.
“Mbona hukukataa mbele yake.”
“Unamuamini yule?”
“Amejuaje kama si wewe uliyemwambia?”
“Lakini si kujua uwezo wako wa kitandani nilimwambia wewe mtundu.”
“Sasa sema moja tumekuja kupeana raha au kuulizana maswali ya kijinga?” Shaka alijifanya kumjia juu Stella baada ya kujua akilegea ameumbuka.
“Kula raha mpenzi wangu.”
“Sasa huo upuuzi umetoka wapi ikiwa ni wewe uliyesema, mimi na wewe nani wa kumlaumu mwenzake?”
“Basi nisamehe mpenzi,” Stella alikuwa mpole.
Shaka alijua Stella ana wasiwasi lakini hana uhakika, aliamini dawa yake ni kumpa penzi mseto la kumrusha akili. Hukuwepo shetani wako alikuwepo. Maskini mtoto wa kike alimaliza maneno yote mdomoni kuusifia uwezo wa Shaka.
“Asante mpenzi sijawahi ila leo ndiyo nimeonja tamu ya penzi, kila kona ya mwili naisikia tamu. Asante mpenzi wangu, chondechonde usimpe mtu utamu huu haki ya nani nitaporwa. Shaka unajua, kweli wewe ni reli nyembamba lakini inabeba treni yenye mabehewa na watu wake.”
Shaka hakujibu kitu kwa vile alijua hawezi kula karanga huku anapiga mluzi, alinyamaza kimya na kuwakusanya mabeki na kuachia shuti kali lililomfanya Stella apige kelele na kwenda juu, aliporudi chini alitulia na kutembeza mikono hewani kama anataka kudaka kitu.
                                                            ***
Nje ya hoteli, Diana aliteseka akiamini Stella alikuwa akifaidi mavituz ya Shaka,  miguu ilikuwa haitulii wadudu wadogowadogo walimtesa, alijikuta akiteseka hata hamu ya kuendelea kuwa pale hakuwa nayo zaidi na yeye kumpata mtu kama Shaka ili ampunguze muwasho wa ulimi usiokunwa kwa vidole.
Alijitahidi kuvumilia kwa saa moja lakini hakumuona mtu akitokea zaidi ya kuendelea kupigwa na baridi huku akikumbuka machejo ya Shaka akiamini lazima shoga yake hatakubali bao moja kama mguu wa jini lazima atataka kichane cha ndizi na kuzidi kumuweka lindo.
Aliamini hawawezi kutoka mapema hasa baada ya kuonja tamu ya Shaka na kujua siri inayomfanya shoga yake kuingia kichwakichwa na kumng’ang’ania kama ruba.
Moyoni aliapa kulipa kisasi kwa Stella kufanya mambo ambayo yatamfanya Shaka amsahau shoga yake siku wakikutana. Aliamini kabisa shoga yake si mjanja katika mambo ya kitandani kama yeye kwa sababu ya geti kali. Kila alivyokuwa akijiuliza uwezo wa Shaka na umbile lake alichanganyikiwa.
 Aliwazidi wanaume wengi wenye maumbile na umri mkubwa aliofanya nao mapenzi wakiwa wamelewa na kushindwa kumkidhi haja zake na yeye kwa vile huwa anataka fedha kujikuta akifa kizungu na tai shingoni lakini mara nyingi hupakwa shombo tu.
Aliamini siku akimtia mikononi Shaka atahakikisha na yeye anakamuliwa zote za muda aliokuwa naye mbali. Muda nao ulikuwa ukikatika kama hauna akili nzuri hakuonekana Stella wala kivuli chake.
Aliamua kumpigia simu ambayo iliita mpaka inakatika bila kupokewa alirudia zaidi ya mara tano. Mwisho wake ilizimwa kabisa, kitendo kile muudhi sana na kuona amedharauliwa na kujiuliza kama mpaka simu imezimwa ina maanisha hawatoki mapema amenogewa na kuona simu yake kero heri angepokea na kumweleza anatoka saa ngapi.
Stella aliamua kuongeza nusu saa kama itavuka hatakuwa na silimile zaidi ya kuondoka. Lakini saa nzima ilipita bila kuonekana alijaribu tena kupiga simu lakini haikupatikana aliamua kuondoka.
 Ndani ndiyo kwanza Stella alikuwa akishtuka usingizini na kumkuta Shaka amelala lakini bakora ilikuwa juu kama mkungu wa ndizi, saa ya mkononi ilimuonesha muda umekwenda na kamuweka shoga yake saa mbili zaidi ya makubaliano.
Alijifikiria waondoke au aendelee, lakini hamu ilikuwa kubwa kuliko woga wa kurudi nyumbani. Alimshtua Shaka aliyekuwa usingizini, alipoamka na kuona muda umekwenda alimuuliza:
“Vipi ndo tunaondoka?”
“Shaka umenichoka?” Stella alimuuliza Shaka huku akimshika kifuani.
“Vipi tena mpenzi?”
“Hivi Shaka hujisikii kuwa na mimi, tuna muda gani hujanipa haki yangu mimi mkeo?”
“Ni muda mrefu lakini sipendi upate tatizo kwa ajili yangu.”
“Tatizo gani Shaka, hakuna tatizo lolote.”
“Na kuhusu Diana?”
“Shaka unamjua Diana kuliko mimi?”
“Kumjua siyo sababu zaidi ya makubaliano yenu, siku zote tunakutana peke yetu kama umemleta lazima uheshimu makubaliano.”
“Nikubaliana na wewe lakini mimi na Diana tunajuana.”
“Mmh! Kumbe huo ndiyo mtindo wenu.”
“Mtindo gani?”
“Na yeye akienda kwa mwanaume wake unamsindikiza?”
“Hata siku moja.”
“Lakini wewe huwa anakusindikiza.”
“Mara nyingi.”
“Kwa rafiki zako.”
“Shaka hayo maneno gani, unaniona malaya siyo kwa kukuvulia nguo yangu ya ndani siyo?” Stella aling’aka
“Hilo si jibu, nijibu nililokuuliza,” Shaka kwa mara ya kwanza alimkazia Stella sauti ya kiume Stella.
“Siyo hivyo Shaka, mara nyingi ninapokuwa na wewe huwa anajua nipo wapi hunipitia na kunisindikiza nyumbani, kwa vile ni shoga yangu humuamini kuwa nimepitia kwao.”
“Bado sijakuelewa, inaonekana hii ndiyo tabia yenu?”
“Tabia gani tena baby mbona najuta kulizua.”
“Siyo kulizua nafahamu kabisa mtindo huu haukuanza leo kwa vile sikukuta msichana.”
“Mungu wangu, yaani umefika huko?”
“Mimi nani yako?”
“Mume wangu.”

MTUNZI: DK. AMBE
Endelea kulike ==>www.facebook.com/2jiachie

ITAENDELEASIKU YA KESHO

No comments

Powered by Blogger.