ad

ad

MH! MISSED CALL YA SHEMEJI - 05


ILIPOISHIA IJUMAA WIKIENDA:
Nawewe unayaweza mama najuta kumfahamu mdogo wako kabla yako, wewe ndiye ulipaswa uwe mke wangu, unipikie, unifulie, uniogeshe na unifanyie mambo mazuri kama haya kila ninapohitaji. Beka alimwambia shemejiye, wakachela
 “Mimi naona  hujaamua tu kufanya hivyo…hata leo ukitaka kumuacha yule chakubimbi wako unaweza…tena ukimuacha nitafurahi sana,” shemeji yake alimwambia Beka.
SASA JIONEZE MWENYEWE…
“Mimi naweza kumfanyia mizengwe mpaka akimbie halafu uchukue nafasi yake tule nanasi kwa nafasi na si kwa kujibanabana!” Beka alimwambia shemeji.
KAMA UNA NDOTO YA KUNUNUA GARI BASI KILIKI TANGAZO HILI CHINI UJIONEE
Baada ya kutoa kauli hiyo, shemejiye alikenua meno yote thelathini na mbili nje, akamkumbatia Beka, akambusu midomoni, mume huyo wa mdogo wake akachaji tena, akampa mambo.
Walipomaliza kufurahishana, waliingia bafuni wakaogeshana, wakavaa nguo ndipo Beka akamshauri shemejiye huyo abaki pale kwa muda ili yeye atangulie nyumbani.
Kufuatia shemejiye huyo kufurahishwa na penzi tamu la mume wa mdogo wake, hakuwa na neno alimruhusu kiroho safi, walibusiana na Beka akashika njia kuelekea kwake.
Alipofika alijifanya kushtuka kumkuta mkewe akiwa amejikunyata nje, akamuuliza kulikoni?
“Kila nikikuambia dada yangu hajatulia ndiyo maana kaachwa na mumewe unakuwa upande wake, sasa kaondoka hapa nyumbani bila kuaga mbaya zaidi kaenda kwenye michepuko yake na funguo,” mke wa Beka alimwambia mumewe.
“Inamaana umetafuta kila mahali hujaziona?” Beka alimuuliza mkewe.
“Ndiyo maana yake, wewe unafikiri mimi napenda kukaa hapa nje?” mkewe alimuuliza.
Baada ya Beka kuambiwa hivyo, alijongea kwenye zulia la mlangoni akalifunua na kutoa funguo, mkewe akapigwa na butwaa.
“Si huu hapa,” alisema Beka akimwonesha mkewe.
“Khaa! Au we ulijua funguo iko hapa nini? Mliwasiliana au mlikuwa wote?” aliuliza Aisha huku akimwangalia mumewe kwa macho yaliyojaa maswali kibao na mshangao juu…
“Hapana, huwa najua wengi wanapoondoka majumbani kama kuna wengine watakuja funguo wanaweka chini ya kapeti, we hulijui hilo?”
“Mimi silijui hilo, nina wasiwasi kwamba huenda alikwambia au mlikuwa pamoja.”
“Hapana mke wangu. Mimi nilijaribu tu. Labda kesi ya msingi kwake iwe ya kumpigia simu halafu hapokei na kama atakuja itabidi nimpe masharti ya jinsi ya kuishi hapa nyumbani kwangu, anatakiwa kufuata sheria za hapa na si vinginevyo anavyotaka yeye.”
Kwa maneno hayo ya mume wake, kidogo Aisha alionekana kuelewaelewa, lakini kabla hajafumbua kinywa, dada yake aliingia…
“Dada ulikuwa wapi na kwa nini nakupigia simu hupokei wakati unajua funguo umezificha mahali?” Aisha alikuja juu…
“Sasa kama funguo ningekuwa nimezificha kweli ningewakuta ndani?”
“Hayo ndiyo majibu yako dada angu?”
“Umeyataka mwenyewe Aisha, kuniuliza .”
Beka alipopata nafasi ya kukaa peke yake alianza kumwona shemeji yake ni tatizo kwani hata kama kweli wanaiba lakini ni kwa nini dada mtu amseme vibaya mdogo wake?
“Kwanza ilitakiwa awe mtulivu sana na mpole maana yeye ni dada mtu, angekuwa mdogo mtu ndiyo anafanya hivyo sawa,” aliwaza sana Beka.
***
Mwezi mmoja na  nusu mbele, siku hiyo shemeji mtu huyo alimtumia meseji shemejiye Beka akimuuliza kama wanaweza kuonana…
“Kuna nini kwani dear?” aliuliza Beka…
“Kuna kitu kizuri sana nataka kukwambia mpenzi wangu jamani.”
“Kama nini?”
“He! Kwani hutaki kukutana na mimi siyo?”
“Niko tayari, ila wewe tu. Ninyetishie basi.”
“Nikunyetishie nini bwana, we tulia. Niambie tuonane wapi?”
“Basi jioni ya saa kumi, palepale pa juzi.”
“Sawa, pale ni mwao najua na mambo mengine nitapata.”
“Acha mambo yako wewe! Mambo kama yapi?”
“Si yale baby bwana na wewe, unajifanya hujui siyo? Unajua kila nikikumbuka tulichoofanya kwenye sita kwa sita kule gesti damu zinanikimbia kwa sana mwilini, natamani tena iwe sasa hivi.”
“Teh! Teh! Teh!” Beka aliishia kucheka kwenye meseji kisha akamwambia shemeji yake…
“Lakini mke wangu unazifuta hizi meseji au unaziacha ili uziangalie kama shoo ya muziki?”
“Aaa mume wangu bwana! Ina maana mimi ni mtoto mdogo kama mkeo?”
***
Muda wa ahadi ulifika, dada wa Aisha alijiandaa akaondoka akiwa ameweka funguo chini ya kapeti kama alivyofanya siku ya kwanza.
“Na leo kama atarudi na kutoziona funguo itakuwa shauri yake...ngoja nikampe raha mumewe, mjini hapa ukilala wenzako hatulazi damu,” dada wa Aisha alijisemea moyoni wakati akielekea katika gesti waliyokuwa wakikutania na Beka.
Akiwa anaelekea huko gesti, alimtumia meseji Beka naye akamwambia achukue chumba akifika atalipa. Baadaye Beka naye alifika, akalipia chumba.
Ndani ya chumba, Beka alipokelewa na mabusu kibao huku shemeji yake huyo akimchagiza na maneno ya nakupenda sana baby, sitaki kukupoteza na mengineyo mengi yenye kujazwa na mahaba.
“Mimi pia baby…mimi pia baby,” ndiyo yalikuwa majibu ya Beka kwa shemeji yake huyo.
“Enhe, katika yote tutakayoyafanya leo au muda huu kwanza nataka uniambie hicho ulichoniitia.”
Shemeji mtu huyo alicheka kwanza kisha akawa siriasi, akafunguka …
“Baby nimenasa.”
Beka kwanza hakuelewa, akahisi kama alichokisikia amekitafsiri vingine, akamuuliza…
“Unasema?”
“Nasema mwenzio nimenasa ujauzito, maana nimepitiliza.”
“Una maana gani?”
“Nina ujauzito wako bwana, acha mambo yako wewe.”
 He! Shemeji! Una unini wangu?”
“Ujauzito.”
“He! Kwa hiyo?”
“Kwa hiyo nini shemeji, wewe si ndiye mhusika!”
“Ina maana upo tayari kuzaa?”
“Tatizo liko wapi?”
“Kuzaa na mimi?”
“Mimi sioni shida.”
“Ukitoa mtoto yupo kama mimi mtupu?”
“Haiwezekani hata siku moja.”
“Mh! Hapana, tutoe shemeji.”

Kutoa! Sisi tuliapishwa na baba, mtu akipata mimba akitoa anakufa, hajakwambia mkeo?” alisema dada wa Aisha huku akijing’atang’ata midomo.
Beka hakuwa tayari kuzaa na shemeji yake huyo hata kama walikubaliana kula uroda. Kwake kuzaa na shemeji yake ilikuwa ni kupitiliza kwa kufuru jambo ambalo aliamini linaweza kumpa wakati mgumu katika maisha  ya kifamilia…
“Yaani shemeji itakuwa ngumu sana wewe kuzaa na mimi halafu…”
“Hata mimi itakuwa ngumu sana kutoa hii mimba. Hivi  kama ulikuwa hutaki kuzaa na mimi kwa nini hukuniambia mapema?”
“Shemeji kwani hukujua?”
“Kwamba?”
“Mimi na wewe hatuwezi kuzaa!”
“Tunaweza, sii hutaki! Au hatuwezi kivipi wakati mimi tayari nina mimba yako.”
Beka aliangalia pembeni, shemeji yake akamfuata na kumshikashika sehemu mbalimbali za mwili na kumfanya Beka kusisimka…
“Una…jua she…m tati…zo wewe hu…jui tu, mdo..go wako…ana…” alisema Beka huku akisisimka mwili kutokana na kushikwashikwa na shemejiye mwilini. Alihisi kuchanganyikiwa.
Shemeji mtu huyo naye alijua Beka ameshaingiliwa akili hivyo akazidisha kujituma ili kuingia kwenye hatua nyingine na kuisahau ile ya kwanza ya madai ya mimba…
“Shemeji…”
“Mmh!” Beka aliitika kwa sauti ya chini sana huku macho yakiwa hayaoni sawasawa.
“Unataka nini?”
“Unataka unipe nini wewe?”
“Chochote unachokitaka wewe.”
“Sawa na wewe nipe chochote unachotaka kunipa.”
Mazungumzo yote hayo yaliendelea huku kila mmoja akiwa tayari amewaka moto, hakuna kitu mbele yao zaidi ya mahaba.
Shemeji alimvua nguo Beka huku wakiendelea kusemeshana maneno mbalimbali yenye kuhamasishana zaidi kimahaba mpaka wakajikuta wote hawana nguo kitandani wakaingia mechini..!
***
Ilikuwa siku ya Jumapili, Aisha alikuwa nyumbani, mumewe pia. Aisha alikuwa akizungumza na mumewe kuhusu mambo mbalimbali ya maisha, ghafla dada wa Aisha alikatiza mbele yao akitokea chumbani kwake kwenda bafuni huku akikimbia akiwa amejishika tumbo na kujipigapiga kifuani kama vile anasikia maumivu…
“Dada nini tena?” Aisha aliuliza akimfuatilia kwa macho.
Beka moyo ulimlipuka, alijua tayari kinakaribia kunuka kwani dalili zile za shemeji yake ni za ujauzito wa wazi kabisa…
“Ngoja niende nikamcheki dada,” alisema Aisha.
“Ukamcheki nini sasa wakati mtu mwenyewe anaonesha hataki kusema?”

Atasema tu, si ajabu anaumwa sana.”
Aisha alikwenda bafuni akakutana na matapishi kibao huku dada yake amechuchumaa…
“Dada, ni nini?”
“Naumwa.”
“Nini zaidi?”
“Nahisi malaria.”
“Malaria au mimba dada?”
“Malaria, mimba niitoe wapi mimi?”
“Dada angalia sana na safarisafari zako hizo, kapime dada.”
“Aisha, mbona unanikosea adabu dada yako. Maswali gani hayo kwangu?”
“Sahamani sana dada,” alisema Aisha huku akiondoka kurudi sebuleni.
***
Usiku wa manane, Beka aliamka na kukosa usingizi kabisa. Akaanza kukumbuka picha ya shemeji yake kupita mbio mbele yake na kukimbilia bafuni. Akakumbuka maneno ya mke wake baada ya kurudi bafuni…
“Ana nini?”
“Mh! Mi nahisi ni mjamzito huyu!”
“Yeye kasema mwenyewe?”
“Hajasema, anasingizia homa.”
“Labda ni homa kweli.”
“Homa si angetapika nyongo, huyu kanasa. Na hii yote ni matokeo ya safari zake za kutoeleweka, yamemkuta sasa.”
“Da! Shemeji naye kumbe yupo?”
Beka alijikuta mapigo ya moyo yakimwenda kwa kasi ya ajabu…

Ile mimba lazima itoke. Nikisema iendelee kubaki nitaumbuka,” Beka alijikuta akisema kwa sauti…
“Unasemaje Beka?” mkewe alimuuliza kwa sauti iliyotoka kuamka ghafla.
“Aaa! Nilikuwa naota tu.”
“Sasa kama kuota ndiyo unaota mimbamimba?”
“Sijaota mimba, nimeota miiba. Nimeota kuna rafiki yangu amechomwa na miba, sasa anataka kutolewa.”
“Tuambiane mwenzetu maana tayari humu ndani tuna mjamzito, isijekuwa unamuotea yeye.”
“Aaah! Wapi! Yaani mimi niote ndoto ya mtu mwingine?”
“Kwani haiwezekani?”
Mara simu ya Beka ilitoa mlio wa meseji kuingia, Aisha akashtuka na kuuliza…
“Nani huyo saa hizi?”
Beka pia alishtuka. Alijua kwa swali la mkewe ina maana akishaisoma meseji hiyo lazima aseme ni nani kaituma. Sasa je, kama itakuwa imetumwa na shemeji mtu?
“Sijui nani?” alisema Beka akitaka kupotezea kusoma…
“Hebu msome tumjue huyo anataka nini usiku huu na waume za watu?” “Je, unajua nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma siku ya kesho.
https://www.facebook.com/2jiachie?ref_type=bookmark

No comments

Powered by Blogger.