ad

ad

Kumbe Vikiungwa Vitamu - 09




 ILIPOISHIA
“Manka kwa nini ulinitenda?”
“Kivipi mpenzi?”
“Vitu hivi mbona hukunipa mwanzo?”
“Mpenzi vilikuwa havijaungwa, hata vya chukuchuku havikuiva.”
“Hapana...hapana...sikubali.”
“Hukubali nini tena mpenzi?”
“Siwezi kula nisishibe heri nisipewe.”
“Mateja leo utakula mpaka utasaza nipo kwa ajili yako.”
“Na baada ya leo?”
“Mi nipo tu.”

“Hapana..hapana ...lazima nikuoe.”

“Na mchumba wako?”

“Wewe ndiye uliyekuwa mchumba wangu.”

“Kama nilikuwa mchumba wako kwa nini uliniacha?”

 Huwezi kuamini wakati tukizungumza hivyo kilimo kiliendelea huku Mateja akishinda kukaa chini kama kakalia moto.
TUSAPOTI KWA KUTEMBELEA HILI TANGAZO
“Vipi?” Nilimuuliza huku nikimtazama usoni kwa jicho lilililegea kama mtu mwenye usingizi mzito.

“Mm..mm..mmh,” Mateja aligugumia kama dume la panya kwenye ghala la mahindi.

Baada ya muda maskini mateja machozi yasiyo na kilio yalimtoka, niliyahifadhi hakugusa chini.

“Asante Manka...asante mpenzi.”

Mtoto wa kike sifa hazikunivimbisha kichwa niliuchukua mpini na kuurudisha kwenye jembe kilimo kiliendelea. Mmh, kweli kila kiumbe na sehemu zake, kurudisha mpini kwenye jembe kulikuwa kama kumtupia samaki majini. Mateja alikuja juu kama moto wa kifuu kila nilipotaka kumtuliza ndivyo raha zilivyogonga kila kona ya mwili na kujikuta nikiwacha autawale mchezo.


Nilifika kipindi duniani nikawa sipo mbinguni sipo nikawa naelea kati, nakiri sikujua kilichokuwa kikiendelea zaidi ya kuhisi kama mtu kanivua nguvu zote mwilini kilichoendelea sikujua. Niliposhtuka nilijikuta nimelala pembeni ya Mateja ambaye alikuwa hajitambua kwa usingizi mzito.

Kilinichonishangaza kujikuta sote tumo ndani ya shuka moja, nilijiuliza inawezekana Mateja ndiye aliyenifunika. Nilipotaka kunyanyuka nilihisi kama kizungungu nilijirudisha kulala. Wakati nataka kufumba macho nilisikia naitwa.

“Manka...Manka,” niliposikiliza vizuri niligundua ni Bi Shuu.

“Abee.”

“Amka ujimwagie maji.”

“Sina nguvu.”

“Jitahidi hivyo hivyo.”

Nilijinyanyua kwa kuzilazimisha miguu ikiwa haina nguvu, nilijizoazoa  na kwenda kujimwagia maji, Bi Shuu maji alikwisha yapeleka bafuni. Nilioga maji yaliyokuwa ya baridi sijui aliyatoa kwenye friji. Baada ya kujimwagia maji mwili ulichangamka kidogo, hapo ndipo nilipoanza kuisikia njaa.

“Manka kamuamshe na mwenzako naye akajimwagie maji ili mle pamoja”

“Kwa saa ngapi sasa”

“Saa sita kasoro.”

“Mtume!”

Nilikwenda kumuamsha Mateja aliyekuwa akikoroma ilionekana kalinyekarinde lilimpeleka puta na kujikuta akipoteza nguvu nyingi. Inawezekana kabisa alijua ni yule Manka wa mwaka 47 na kuingia kichwa kichwa matokeo kanyolewa bila maji.

Kila nilipomtikisa alionekana yupo hoi kwa kugeuka kama umekufa, niliendelea kumtikisa.

“Mateja..Mateja.”

“Mmh.”

“Amka.”

“Niache nilale kidogo.”

“Najua umechoka, amka ujimwagie maji upate nguvu.”

“Manka naomba nipumzike nimechoka sana.”

“Matejaaaa, hebu amka.”

Nilimwambia huku nikimshika mkono na kunyanyua, alinyanyuka na kukaa kitako kitandani. Akiwa kama mtu aliyekunywa pombe ambayo ilikuwa bado kichwani, aliinama mkono mmoja alishika kitandani na mwingine kichwani. Sikutaka kumpa nafasi nilimsimamisha na kumfunga upande wa kanga.

Huwezi kuamini nilivyokuwa nimechoka bila kuelekezwa na Bi Shuu nisingeweza kuyafanya yale. Maji ya baridi niliyojimwagia ndiyo yaliyonipa nguvu, nilimshika mkono mpaka bafuni ambako nilikuta tayari Bi Shuu ameisha tayarisha maji ya baridi.

Kwa kuwa nilijua ubaridi  wa maji Mateja atauogopa nilipomtoa kanga nimwagia kwa kumshtukiza kama makopo mawili. Japo alilalamika lakini alinieleza kweli maji yale yameupa tena nguvu mwili wake. Alimuongeza maji mengine na kuufanya mwilini wake uchangamke zaidi.

Alipomaliza kujimwagia maji ya baridi tulirudi ndani, sikuamini macho yangu kukuta Bi Shuu amekwisha andaa chakula mezani kukiwa na kila kitu. Muda wa Mateja kujimwagia maji, yeye aliutumia kuandaa chakula. Yaani sijui niseme nini, nimekutana na watu wengi lakini Bi Shuu kiboko.

Japo usiku ulikuwa mkubwa lakini mama wa watu hakulala alikwenda sambamba na mimi. Kilichonishangaza baada ya mtinange na kupitiwa usingizi nilijiuliza yeye alikuwa wapi? Kama sisi tulilala kwa zaidi ya masaa matatu yeye muda huo alikuwa anafanya nini?

Mateja baada ya kuona nilimsikia akisema.

“Manka umejuaje kama nina njaa, maana hapa nahisi tumbo jeupe.”

Kwa vile na mimi nilikuwa na njaa tulivamia wote mezani kukishambulia chakula kilichokuwa kimepikwa kwa ustadi wa hali ya juu na Bi Shuu. Tukiwa mezani baada ya kufunua kawa lililikuwa na maneno RAHA YA MUWASHO UKUNWE . Ajabu ya Mungu kawa lile lilionekana jipya halijawahi kutumika, baada ya kulifunua harufu nzuri ya chakula ilijaa puani mwetu. Nilimnawisha mikono kisha nilimkaribisha kama nimepika mie.

“Karibu mpenzi.”

“Asante,’” Mateja alijibu huku akijipakulia kwenye sahani yake, wakati anaweka kijiko cha kwanza nilisikia kitu kikigongwa dirishani. Ilionesha kuna kosa nimefanya. Nilinyanyuka haraka huku nikisema.

“Samahani dear nakuja,” nilitoka nje na kukutana na Bi Shuu.

“Vipi Bi Shuu?”

“Manka nilikueleza nini?”

“Kuhusu nini?”

“Mwanaume kama mtoto asiguse kitu kazi yote ifanye wewe.”

“Ulikuwa una maana gani?”

“Asijipakulie, mpakulie ikiwezekana hata vijiko vya awali mlishe kisha mwache ale mwenyewe.”

“Nimekulewa,” nilimjibu bila kusubiri maelezo mengine kumuwahi Mateja asijipakulie zaidi. Nilipofika nilikuta ndio anataka kuongeza kijiko cha tatu. Nilikidaka kijiko na kusema.

“Mpenzi kwa nini usumbuke wakati nipo.”

“Aah, si kila kitu ukifanye.”

“Hapana wewe ni mgeni wangu, kila kitu mimi ndiye dereva.”

“Haya mama.”

Nilimpakulia chakula cha kiasi kisha nilimuwekea mchuzi na kipande cha ndizi, tonge la kwanza nililikusanya kisha nilimlisha huku nikiweka mkono chini ya kidevu kuzuia punje ya wali isianguke. Baada ya kulisha nilimsubiri atafune ili nimuongeze tonge lingine nami nianze kula. Baada ya kutafuna kwa muda nilimsikia aliguna kitu kilichonitisha na kuwa na wasi wasi huenda chakula si kizuri.

“Vipi mpenzi?”

“Mmh, chakula kitamu kweli kweli, sijawahi kula chakula kitamu kama hiki, kama nikikuoa na kula hivi kila siku nitenenepa mlangoni nitakuwa sipiti.”

“Asante mume wangu,” nilijibu makusudi, moyoni niliisifia kazi nzuri ya Bi Shuu.

“Manka,” Mateja aliniita huku akivuta glasi ya maji iliyokuwa pembeni.

“Abee.”

“Manka mbona leo naona kama nipo ndotoni?”

“Kivipi?”

“Mbona siku za nyuma hukunifanyia mambo kama haya, mapenzi ya ukweli na chakula kitamu kweli kweli.”

“Vimeungwa.”

“Una maana gani?”

“Mateja mimi ni Manka mpya.”

“Una maana gani?”

“Ulichokiona kazi kubwa ya Bi Shuu.”

“Bado umeniacha njia panda Bi Shuu amefanya nini?”

Nilimuelezea bila kumficha kazi kubwa ya Bi Shuu kuniunga na leo kuvionjwa akaviona vitamu.

“Upo hapo baba?”

“Mmh, nimekubali kweli aliomba likizo yenye mafanikio.”

“Basi habari ndio hiyo.”

Baada ya chakula tulirudi kuoga tena kisha tulipanda kitandani kulala hakuna aliyekuwa na hamu na mwenzake tulipeana migongo mpaka asubuhi. Mlio wa dirisha uliniamsha toka kwenye usingizi mzito, jicho langu lilitua kwenye saa ya ukutani kunionesha ni saa kumi na moja alfajiri.

Nilijinyanyua kivivu na kwenda hadi mlangoni kumsikiliza Bi Shuu alitaka kunielaza nini, nilifungua mlango huku nikifikicha macho kutokana na kuzingirwa na usingizi ulioambatana na uchovu wa mwili. Nilikumbuka usiku wa jana nilitumia nguvu nyingi ili kumuonesha Mateja mimi ni nani.

Nakumbuka kuna kipindi niliona kama chini nachochewa kuni jinsi moto ulivyokuwa ukiwaka. Lakini nilikumbuka maneno ya Bi Shuu sifa kubwa ya mwanamke kwa mwanaume ni uvumilivu na kutokukubali kushindwa mapema hata siku ya kwanza unapotaka kuandika CV.

Baada ya kufungua mlango nilikutana na Bi Shuu akiwa na upande wa shuka.

“Shikamoo Bi Shuu.”

“Marahaba mama Shughuli.”

“Mmh! Bi Shuu jina gani tena hilo.”

“Kwani uongo shughuli unaiweza, mwana wewe temea chini.”

“Aii jamani,” nilijikuta nikiona aibu kwa kujua kila nilichokifanya Bi Shuu alikiona ‘live’ bila chenga.

“Sasa Manka sicho nilichokuamshia, vipi ushampa cha alfajiri?”

“Kipi hicho?”

“Ooh, kweli hili sikukuelekeza, raha ya mapenzi ukilala na mwanaume mpe cha asubuhi ili kiwachangamshe, kijasho kikiwatoka mkaoge mjiandae kwenda kazini.”

“Si tutachoka sana.”

“Uchoke nini, hiyo sawa na kuzimua baada ya kulala na hang over asubuhi ukizimua unajiona sawa hata uzito wa kichwa unapotea sawa na kupata cha asubuhi.”

“Mmh! Sawa wacha basi nifanye hivyo.”

Niliagana na Bi Shuu na kurudi ndani, Mateja alikuwa bado amelala nilimshtua kwa kumpa mshikemshike wa kuvamia shamba lake kwa kuufukua muhogo taratibu kitu kilichomshtua kunikuta nipo shambani na tayari  muhogo nilikuwa nimeisha ufukua upo mkononi.

“Vipi mpenzi?” aliniuliza kwa sauti ya usingizi.

“Kawaida tu.”

“Niache nilale nimechoka.”

“Kumekucha mpenzi tunazimua kisha tunakwenda kuoga.”
ITAENDELEA KESHOOOOOOOOOOO

No comments

Powered by Blogger.